HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 29, 2017

Bosi mpya Zantel aahidi makubwa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu Zantel, Sherif El Barbary, kifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Rasilimali Watu, Joanitha Mrengo. (Picha na Francis Dande). 

NA MWANDISHI WETU

WATEJA wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu Zantel wataweza kuendana na mabadiliko ya kidunia katika sekta ya Mawasiliano kupitia mfumo bora wa data na sauti baada ya kumalizika kwa kazi ya uboreshaji wa mfumo mpya wa mtandao wa kisasa kuongeza ubora wa bidhaa na huduma kuelekea mwaka 2018.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Sherif El Barbary, alisema amedhamitria  amedhamiria kuboresha ubora wa mtandao huo na kuwafikia wateja nchi nzima na kuenea sehemu kubwa Tanzania kwa kutoa huduma bora na kuifanya Zantel kukua katika soko la ushindani kwenye sekta ya Mawasiliano.

“Tunatarajia kuwafuata wateja wetu walipo na kuwapa kile wanachostahili ili kuhakikisha kwamba wanamudu gharama na kuongeza kipato kupitia malengo na dira yetu,” alisema.

El Barbary alisema Zantel ipo katika hatua za mwisho kumalizia uboreshaji wa mfumo wa mtandao na haina shaka kuwa, imekuwa kampuni ambayo inatoa huduma bora za mtandao wa data nchini katika mikoa zaidi ya 22 ambapo wanapata mfumo ulio na kasi ya 4G, huku malengo yake yakiifanya kuongoza soko na mfumo mpya wa kisasa na kidigitali.

Alisisitiza, Zantel itataendelea kushirikiana na Serikali ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa kila nyanja.  “Tumetengeneza zaidi ya ajira 5,000 nchi nzima. Hizi ni zile rasmi na zisizo rasmi kupitia mfumo wa EzyPesa ambapo una takribani mawakala 2,500. 

“Pia tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi wetu wa Zantel.  Hii ni tofauti na wasambazaji wetu ambao wamekuwa wakifanya kazi na watu mbalimbali kusambaza bidhaa na huduma zetu,” aliongeza.

Kwa upande wa huduma za kijamii, Zantel imekuwa ikishiriki kupitia M-Health ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali ambayo imekuwa ikisaidia kuimarisha sekta ya afya kwa kuboresha huduma bora za afya hususani za mama wajamzito na watoto. Kwa kuunganisha mifumo ya intaneti ya data imekuwa njia rahisi ya kutoa elimu kupitia kampeni mbalimbali.

El Barbary, ni mwenye uzoefu wa takriban miaka 20 katika sekta ya Mawasiliano, akishika nafasi mbalimbali za juu za utawala katika taasisi za kimataifa.

Kabla ya kutua Zantel, El Barbary alikuwa Ofisa Ufundi na Mawasiliano Tigo nchini Chad tangu Machi, 2016, amefanya kazi kama msimamizi wa masuala ya mtandao na shughuli za IT na ufuatiliaji. Pia amekuwa kaimu Meneja Mkuu nchini Chad.

No comments:

Post a Comment

Pages