HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 22, 2017

HOTELI ZAASWA KUBADILIKA ILI KUENDANA NA SOKO

Na Jumia Travel Tanzania

Kwa mujibu wa baadhi ya wamiliki wa hoteli za jijini Dar es Salaam wanadai kwamba hali ya biashara ni ngumu kidogo ukilinganisha na miaka miwili iliyopita. Na hiyo ni kutokana na sababu kwamba baadhi ya huduma ambazo walikuwa akizitegemea sana kupungua, ikiwemo kukodisha kumbi kwa ajili ya mikutano.

Kupitia kampeni yake ya kuhamasisha maeneo mbalimbali ya vivutio nchini Tanzania, Jumia Travel imekuwa ikitembelea hoteli tofuati na kufanya mahojiano. Katika zoezi hilo wamiliki na mameneja wa hoteli huulizwa juu ya masuala mbalimbali kuhusu

mwenendo wa biashara na mazingira kwa ujumla.


Baada ya kuangazia maeneo na hoteli tofauti za visiwani Zanzibar, jiji la Dar es Salaam nalo limepata fursa hiyo. Yafuatayo ni mahojiano na Bi. Lusinda ambaye ni Meneja Mkuu wa hoteli ya Slipway ya jijini Dar es Salaam:


JT: Unaizungumziaje hoteli yako?

Lusinda: Ni hoteli ya kifahari yenye vyumba 72 tofauti kwa ajili ya wageni ikiwa inapatikana eneo la Peninsula ya Msasani. Mbali na kutoa mandhari nzuri ya bahari ya Hindi pia tumezungukwa na maduka kadhaa kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa mbalimbali za asili.


JT: Ni wageni wa aina gani hutembelea zaidi hotelini kwenu? Je hupendelea/kuulizia shughuli gani zaidi?


Lusinda: Mara nyingi tunapokea wageni kutoka nje ya nchi ukilinganisha na wa hapa nyumbani. Tofauti na sehemu zingine, jiji la Dar es Salaam halina vivutio vingi ambavyo wageni wakifika hupenda kuvitembelea. Hivyo basi kutokana na uzoefu wetu

hapa wengi hupendelea kwenda kutembelea Visiwani Zanzibar, pia huulizia sehemu za kwenda kujionea shughuli za kisanaa na kitamaduni.


JT: Unauzungumziaje ukuaji wa utalii wa ndani?

Lusinda: Kwa maoni yangu, ukuaji ni wa kusuasua ukilinganisha na idadi ya wageni wanaokuja nchini na kutembelea vivutio vya kitalii. Nadhani zinahitajika jitihada za kutosha katika kuvitangaza vivutio vyetu, kurahisisha gharama pamoja na kubadili dhana nzima juu ya utalii.


JT: Unalizingumziaje jiji la Dar es Salaam kwa upande wa kitalii?

Lusinda: Kwa asilimia kubwa jiji la Dar es Salaam halina sehemu za kutosha kwa ajili ya shughuli za kiutalii bali kutingwa na sehemu za kibiashara. Kwa uzoefu wangu nilionao hapa hotelini, wageni wengi wanaokuja ni kwa ajili ya shughuli za kibiashara. Na baadhi yao hufanya kama ni kituo kwa ajili ya kwenda sehemu

nyingine zenye vivutio vya kitalii kama vile Visiwani Zanzibar, Arusha, Serengeti au Kilimanjaro.


JT: Unaionaje hali ya biashara kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha nyuma? Lusinda: Ni nzuri, kwa hoteli za Dar es Salaam ambapo ni jiji la kibiashara.


Biashara haina msimu kwamba itafika kipindi fulani watu wataacha au kupumzika. Muda wote, majira yote ya mwaka jiji hili limejawa na pilika nyingi za wafanyabiashara. Kwa mfano, sisi hapa tunapokea wageni wengi kuanzia katikati ya


mwanzo wa mwaka yaani Januari mpaka katikati ya mwisho wa mwaka, Disemba. Nimekuwa nikisikia baadhi ya maoni ya wamiliki na mameneja wa hoteli juu ya kubadilika kwa

biashara hususani kupungua kwa huduma ya kumbi za mikutano tofauti na miaka miwili iliyopita kabla ya kuingia serikali mpya. Ninachoweza kusema ni kwamba suala hilo linategemea meneja au mmiliki wa hoteli alijijengea vipi misingi ya biashara yake.

Kama ulikuwa unategemea biashara kwa upande huo ni kweli unaweza kuathirika, lakini kama ulijipanga na kujiimarisha kwenye maeneo mengine natumaini mambo yatakuwa yanakwenda vizuri.


JT: Unadhani mifumo ya mtandaoni ina mchango wowote kwenye sekta ya utalii nchini?

Lusinda: Ndiyo, ina mchango mkubwa tu kwani inasaidia katika kuongeza idadi ya wageni kwenye hoteli. Kutokana na mabadiliko ya tekinolojia, hatuwezi kuwa tunategemea wateja wanaokuja moja kwa moja hotelini. Kwa mfano, hoteli yetu inapokea wageni wengi kutoka nchi za Marekani, Uingereza pamoja na nchi za

Scandinavia (Denmark, Norway, Sweden na Finland).


JT: Unauonaje usharikiano baina ya hoteli yako na Jumia Travel? Je una manufaa yoyote?

Lusinda: Ushirikiano ni mzuri na una manufaa kwetu kwani unatuongezea njia tofauti za kujitangaza zaidi. Jitihada zinahitajika zaidi katika kuhakikisha kwamba wanawafikia wateja wengi zaidi.


Kwa mfano, Tanzania kwa sasa inashuhudia kukua kwa

kasi kwa watu wa daraja la kati ambao wana uwezo kwenye kufanya matumizi. Hivyo basi ni fursa kuwalenga watu wa kundi hili kwa njia tofauti kama vile kubuni huduma na vifurushi vya bei ambazo zitawavutia zaidi.


JT: Kwa kumalizia, una maoni gani juu ya ushindani uliopo kwenye soko kwa sasa ukizingatia hoteli kadhaa mpya zikizidi kuzinduliwa?
Lusinda: Mimi ninaamini kwamba kuna fursa za kutosha kwa kila mmoja wetu kufanya biashara. Kila hoteli ina namna ya kufanya biashara na wateja inaowalenga kutokana na upekee na huduma ilizonazo. Hivyo, dhana ya kwamba kuzidi kufunguliwa kwa

hoteli mpya kutafanya wateja kupungua sidhani kama ina ukweli ndani yake. Cha zaidi ninachokiona kufunguliwa kwa hoteli mpya ni chachu katika ukuaji wa sekta ya utalii nchini na kunatakiwa kuhamasishwa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages