Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya mabadiliko kidogo ya muda
wa kuanza mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Azam FC
na Simba SC.
Mchezo
huo utafanyika kesho Jumamosi Septemba 9, 2017 kwenye Uwanja wa Azam
ulioko Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salam kama ulivyopangwa
awali.
Kuhusu
muda, mchezo huo ulipangwa ufanyike kuanzia saa 1.00 usiku, lakini sasa
utaanza saa 10.00 jioni - uamuzi uliofanyika baada ya kupokea ushauri
kutoka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, chini ya
Mwenyekiti wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda.
Mbali
ya mchezo huo, mechi nyingine ya kesho Jumamosi Septemba 9, mwaka huu
itakuwa ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea uliopangwa
kufanyika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom, zitakuwa Jumapili Septemba 10, mwaka
huu ambako Njombe Mji FC na Young Africans SC zitacheza Uwanja wa
Sabasaba mjini Makambako wakati Mtibwa Sugar FC na Mwadui FC ya
Shinyanga kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Kadhalika
Lipuli FC itacheza na Stand United FC Uwanja wa Samora mjini Iringa
wakati Singida United itacheza na Mbao kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Dodoma.
Pia
Kagera Sugar itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini
Bukoba huku Mbaya City ikiwa wenyeji wa Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja
wa Sokoine mjini Mbeya.
TAARIFA KUHUSU WA WAAMUZI TANZANIA
Kamati
ya Utendaji ya Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT)
ilikuwa na kikao chake cha kwanza kilichofanyika Julai 6, 2017 hapa
jijini Dar es Salaam.
Mambo muhimu yafuatayo yalitolewa uamuzi.
1.
Kumpongeza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Bw. Wallace
Karia na Makamu wa Rais, Bw. Michael Wambura pamoja na Wajumbe wote wa
Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kuchaguliwa kwao.
2.
Tumesimamisha kozi zote kwa waamuzi wapya kuanzia Septemba 7, mwaka
huu. Mitihani iliyokwishafanywa kabla ya Septemba 7, mwaka huu ni halali
na itumwe kwa Katibu Mkuu wa FRAT - Taifa mara moja ikiambatanishwa na
ada zake.
3.
Makatibu wote wa FRAT - Mkoa kwa mikoa yote ya Tanzania Bara
wakumbushwe majukumu yao kwani inaonekana ni kama wamepitiwa ikiwa ni
pamoja na kutuma kwa Katibu Mkuu FRAT - Taifa orodha ya waamuzi wote wa
madaraja yote walio hai kwa kuchezesha na walio hai kiuanachama.
4.
Tumekumbusha waamuzi kuwa na darasa la mara moja kwa wiki lijulikanalo
kama ‘Sunday Class’ madarasa hayo yawe kila Makao Makuu ya Mkoa na Makao
Makuu ya Wilaya.
5.
Tumekubaliana uchaguzi mdogo ufanyike wakati wa mapumziko ya ligi ya
wiki mbili za mwezi Januari. Tayari tumewasiliana na na Kamati ya
Uchaguzi.
6. Kuwaleta pamoja waamuzi (wanachama) wote nchini bila kujali umri.
7. Kuendelea kuzalisha waamuzi wapya toka kwenye shule za sekondari, vyuo na nje ya shule za sekondari na vyuo kwa wenye sifa.
8. Kuboresha mafunzo na upandaji wa madaraja kwa waamuzi wenye madaraja.
9. Kukemea na Kupambana na rushwa kwa waamuzi hadharani kwa kushirikiana na TFF na Takukuru.
10. Kutetea kwa nguvu zote haki za waamuzi.
11. Kuboresha mawasiliano kwa ngazi zote na kwa mwanachama ye yote.
12. FRAT kiwe chama cha mfano kwa wanachama wake kwa kuwa na maadili mema, yanayompendeza Mungu.
13. Misingi kumi ya “FIFA FAIR PLAY” ni msingi wa maendeleo ya mwamuzi.
14. Wote kwa pamoja tukatae rushwa na tuiangamize rushwa kwa maendeleo ya mpira wetu.
……………………………………………………………………..…… ………..……
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment