Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael, akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kuhusu huduma mpya ya simu za mkononi ijulikanayo kama Twende App inayowawezesha wasari kupata huduma ya haraka na usalama ya usafiri wa umma wa Taxi, pikipiki za bodaboda na pikipiki za magurudumu matatu kwa kutumia simu za mkononi. Kulia ni Mkurugenzi wa Twende App, Justin Kashaigili.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Twende App
kuwawezesha wasafiri kupata huduma ya usafiri kupitia simu za mkononi.
Arusha 8 Septembea, 2017-
Kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo
Tanzania imeungana
na kampni inayotoa huduma za usafiri Twende App kuzindua huduma mpya
itakayowezehsa wasafiri kupata huduma bora, ya haraka na uhakika zaidi kupitia
mfumo wa simu za mkononi unaojulikana kama Twende App.
TwendeApp ni mfumo wa kidigitali wa simu za
mkononi unaowezesha wasafiri kutafuta na kupata usafiri wa taxi, pikipiki za
magurudumu mawili (bodaboda) na zile za
magurudumu matatu kupitia simu zao za
mkononi kwa uhakika zaidi na kwa bei nafuu.
Twende App ambayo, tayari inatumika katika
jiji la Dar es salaam, sasa imepanua wigo wake na kufikia miji ya Arusha, Morogoro, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma Iringa na
Mbeya. Kuna mipango ya kusambaza huduma hiyo kwenda Zanzibar, Tanga na Mtwara.
Akizungumza katika uzinduzi wa Wende App
jijini Arusha leo, Meneja Uhusiano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Twende
App inatumia teknologia ya GPS kwa
kutegemea mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo. Hii inawahakikishia watumiaji
huduma ya uhakika, haraka na yenye usalama wa hali ya juu.
‘Kwa sasa magari mengi ya usafiri wa taxi na
bodaboda yamepaki kwenye vijiwe wakisubiri wateja. Twende App itawaunganisha
madereva na wasafiri kwa muda na sehemu sahihi na inayohitajika. Kwa kupakua
mfumio wa Twende App kwenye simu zao za mkononi, wasafiri wataweza kuwasiliana kwa
haraka na madereva wa vyombo vya usafiri wa umma ambao wapo karibu zaidi na
eneo husika ambapo usafiri wenyewe unahitajika.
Hii inaondoa adha ya kutembea
kutafuta usafiri na pia inapunguza muda wa kusubiri usafiri kwani mteja
anawasiliana kwa haraka na chombo cha usafiri kilichokuwa karibu zaidi naye.
Kwa upande wa madereva, Twende App itawaokolea muda, kuwaongezea wateja na
kuongeza mapato kwa kuwa hawahitaji tena
kushinda kijiweni wakisubiri wateja,’ alisema.
‘Wateja
wanaohitaji usafiri wanaweza kuona eneo ambalo madereva wapo kwa kutumia
teknologia ya GPS na mfumo wa Google maps. Baada ya hapa watatuma ombi la
kupata usafiri na moja kwa moja, mtandao huu wa Twende App utamjulisha dereva
aliye karibu zaidi kuhusu ombi hili la usafiri na eneo ambalo msafiri yupo,’aliongeza.
Woinde aliongeza kuwa mfumo huu wa kisasa
unapatikana kupitia simu za kisasa za kupangusa (smartphones), kwa hiyo
utaongeza matumizi ya simu za kisasa nchini ikiwemo matumizi ya mfumo wa
kutumia simu za mkononi kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa mbali mbali.
‘Twende App pia inakuletea matumizi ya Tigo pesa katika
biashara ya usafiri. Hii inaendana na dhana kuu ya Tigo ambayo ni kuongeza
matumizi ya mfumo wa digitali nchini pamoja na kutoa huduma ambazo zinaboresha
na kujibu mahitajiya wateja wake nchini kote. Tunawaasa wateja wetu kujaribu
mfumo huu mpya katika kipindi hiki cha Tigo Fiesta 2017 kama njia bora ya
kwenda na kutoka kwenye matamasha ya msimu huu,’ Woinde alisema.
Mkurugenzi wa Twende App, Justin Kashaigili, alisema
kuwa mfumo huu unatumia madereva na magari ambayo yana leseni halali za udereva
na za biashara, na waliothibitishwa kutokuwa na historia ya uhalifu. Hii
inawahakikishia wasafiri usalama wao. Kwa kushirikiana na Tigo, Twende App pia
inatoa simu za kisasa zaidi ya 1,000 kwa madereva wanaojisajili na Twende App
ili kuwawezesha madereva kufanya biashara zao kwa umakini zaidi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa
Madereva Taxi wa Arusha, Ali Mohammed, aliusifu mfumo huo mpya huku akisema
kuwa utawaongezea kipato, usalama na kuwapa uhakika zaidi katika biashara zao.
‘Kwa
bahati mbaya kumekuwa na matukio ya uhalifu yanayohusu madereva na hata abiria
wa usafiri wa umma. Twende App itasaidia kuondoa hofu baina ya dereva na
msafiri kwani wote wanakuwa wamesajiliwa katika mfumo mmoja kwa hiyo hata
upotevu wa aina yoyote ukitokea, suala la ufuatiliaji linakuwa rahisi,’
alisema.
No comments:
Post a Comment