HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 27, 2017

MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA

  Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu namna mchezo huu wa Tatu Mzuka unavyobadili maisha ya watu,huku akimtaja Rebecca Amos (pichani kulia),mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milio 60,picha shoto ni rafiki wa mshindi wa Tatu Mzuka kwa wiki hii,Agness Swai

Maganga  alisema kuwa Droo inayofanyika mara moja katika Juma si aina pekee ya kupata washindi katika mchezo huu, kwa kuwa kila mtu anapocheza Tatu Mzuka anapata pia nafasi ya kushinda mara 200 ya kiasi alichotumia kucheza kila saa. Droo hizi za kila saa kwa sasa zinatoa washindi ambao wanapata hadi kiasi cha shilingi milioni 300,000 katika Juma, kwa washindi mbalimbali nchini Tanzania.”
 Rebecca Amos (pichani kulia),mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milio 60 za Tatu Mzuka,akitoa ushuhuda wake kuhusiana na mchezo huo na hatimaye nae kuibuka mshindi wa mamilioni.Rebecca amewaasa watu wengine kucheza mchezo huo kwani mmoja wao anaweza akaibuka mshindi na kubadilisha kabisa mfumo wake wa kimaisha kupitia fedha atakazo kuwa ameshinda 
Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Rebecca Amos ,mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 60,mapema leo jijini Dar.

Kwa mara nyingine mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, mchezo unaojinyakulia umaarufu mkubwa nchini Tanzania, umetangaza mshindi wake wa droo kubwa ya Juma la nane ambaye amejishindia kitita cha shilingi za Kitanzania milioni 60. Mshindi huyu si mwingine bali Bi. Rebecca Amos mkazi wa Yombo Vituka, jijini Dar es Salaam. 

Bi Rebecca, mwenye umri wa miaka 22, ameibuka na ushindi huu mnono katika mchezo uliofanyika Jumapili iliyopita na kurushwa mubashara katika televisheni.

Kufuatia zawadi hii ya iliyotolewa Juma hili na aina ya washindi wanaoibuka, mchezo wa Tatu Mzuka ni dhahiri umeendelea kuleta mageuzi makubwa katika eneo la michezo ya Bahati Nasibu hapa nchini. Hii inatokana na aina ya washindi wanaopatikana na pia uwezo Tatu Mzuka kutoa zawadi za washindi zinazofikia kiasi cha shilingi milioni 2 kila saa kwa saa 24 kwa siku. Ushindi huu unatolewa ilhali kiasi cha kushiriki katika mchezo huu kikiwa ni kuanzia shilingi 500 tu huku droo za kusaka washindi zikifanyika kila saa.

Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu namna mchezo huu wa Tatu Mzuka unavyobadili maisha ya watu, Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga alisema; “Droo inayofanyika mara moja katika Juma si aina pekee ya kupata washindi katika mchezo huu kwa kuwa kila mtu anapocheza Tatu Mzuka anapata pia nafasi ya kushinda mara 200 ya kiasi alichotumia kucheza kila saa. Droo hizi za kila saa kwa sasa zinatoa washindi ambao wanapata hadi kiasi cha shilingi milioni 300,000 katika Juma, kwa washindi mbalimbali nchini Tanzania.”

Bw. Maganga pia aliongeza kuwa, “tumeongeza kipengele cha ziada katika Tatu Mzuka ambacho kinaitwa ‘Cheza na Washkaji, shinda na washkaji’. Katika kipengele hiki, mshindi wa droo kubwa anapata pia nafasi ya kutaja majina matatu ya rafiki zake ambao nao hujinyakulia kiasi cha shilingi milioni 1 kila mmoja.”

Bi. Rebecca pia amefanikiwa kutaja majina matatu ya rafiki zake ambao wamejinyakulia kiasi cha shilingi milioni 1 kila mmoja. Washindi hao wa ziada wa Bi. Rebecca walikuwa ni mpenzi wake wa miaka mitano Bw. Ramathan Majiran na marafiki zake wawili tangu shule ya Msingi Agnes na Amina.

Washindi hawa wa nyongeza nao hawakuamini ushindi wao hadi pale fedha za ushindi ziliporushwa katika simu zao. Amina alikimbia kwa furaha kutoa fedha zile na kushangilia akiwa kazishika mkononi huku Agnes alishangaa kuona fedha hizo zikiingia kwenye simu yake kupitia MPESA wakati akipata mlo wa mchana. “Nilijawa furaha kubwa sana ambayo ilinifanya kutoendelea kula,” anasema Agnes.

Bi. Rebecca mshindi wa droo ya nane, ni mama wa motto mmoja ambaye hana ajira kwa sasa. Anaishi na wazazi wake ambao anawategemea kwa kila kitu.

“Nimekuwa na ndoto, ndoto kubwa tu lakini sikuwahi kuota bkuwa ipo siku nitafanikiwa kushika fedha nyingi kiasi hiki. Sasa naweza kuanzisha biashara, kuwasaidia wazazi wangu na pia kuwa na uwezo wa kumhudumia mwanangu. Kipi cha ziada ambacho binadamu anaomba kupata zaidi ya hiki?” Bi. Rebecca alisikika akisema.

No comments:

Post a Comment

Pages