HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2017

RPC LINDI AWAAPISHA GIRL GUIDES 230, WABAKAJI WATOTO SASA KUKIONA

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga (kushoto), akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG. 
 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Macha akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini. 

Na Richard Mwaikenda, Lindi

 JESHI la Polisi limeahidi kushirikiana na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), kuwakamata wanaowanyanyasa na kuwabaka Watoto wa Kike.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga 

katika hafla ya kuwaapisha wanafunzi wa kike 230 waliojiunga na TGGA mkoani Lindi jana.

Hilo siyo ombi bali ni wajibu wa jeshi la Polisi kushirikiana na chama hicho pamoja na jamii kuhakikisha wale wote 

wanaowatendea vitendo vibaya watoto wa kike wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali  za kisheria.

"Msiombe msaada kwetu, bali sisi tunahitaji sana msaada mkubwa kutoka kwenu, kwani huku kwetu watoto wa kike 

wanakuja wakiwa wameharibikiwa, ushauri wenu kwao umesaidia sana," alisema Kamanda Mzinga na kuwataka 

waendelee kutoa elimu hiyo kwenye Tarafa, Kata, Kijiji na vitongoji ili kumkoboa mtoto wa kike.

Kamanda Mzinga, aliipongeza TGGA kwa kitendo cha kuwapatia mafunzo takribani wasichana 1200 ya jinsi ya 

kuepukana na vitendo vibaya vya kubakwa na kupewa mimba, magonja kama vile Ukimwi na ndoa za utotoni.

Akielezea walichonufaika katika wakati wa mafunzo yaliyodumu kwa takribani siku nne, Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa 

Lindi, alisema kuwa waischana walifaidika kwa kupata mafunzo ya ukakamavu, kujiamiini, kuepukana na vikwazo 

mbalimbali wanavyokumbana navyo wakati wa kwenda shule na kurejea nyumbani ikiwemo kurubuniwa kwa kupewa 

mimba za utotoni.

Alitaja mambo mengini waliyonufaika nayo ni ujasiriamali, utunzaji wa mwili, utunzaji wa mazingira, uongozi, maadili, 

kujitolea , kuwa na upendo na uzalendo kwa nchi yao.

Mwenyekiti aliimpongeza Kamanda Mzinga kwa kuwapatia askari wa kike ambaye anafanya kazi nzuri ya kukutana na 

watoto wanaoelezea matatizo yao bila woga baada ya kupata mafunzo ya TGGA, ambapo alidai baadhi ya wanafunzi 

hao wanadiriki kusema wazi kwamba wazazi wao wana tabia ya kutaka kuwabaka.

Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba, aliwaasa wasichana waliopata mafunzo hayo, kulinda kiapo walichokipata 

kwa kuwa watiifu na kuweka mbele uzalendo, awe na imani iliyo thabiti katika maisha yake, nchi yake na Jamii.

"Hivyo basi msilichukulie jambo la kawaida,  libaki mioyoni mwenu mbele ya Mungu na muepukane na ulevi, kutumia 

dawa za kulevya, matumizi mabaya ya mitandao, tunataka muwe na misimamo katika maisha yao yote."Alisema Shaba.

Alisema TGGA ina utaratibu wa kuwaingiza uanachama kuanzia watoto wa miaka mitatu na kuendelea ambapo 

huwapatia  mafunzo ya kujiamini, kujithamini, ujasiriamali na kuipenda nchi yao.

Pia alitangaza  kwa wanachama wao walio likizo na waliomaliza shule wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kuomba 

kujiunga na programu ya Yess kwenda nje ya nchi kupata mafunzo ya uongozi, utamaduni na maadili katika nchi tano 

wanachama kwa ufadhili wa Makao Makuu ya Girl Guides ulimwenguni.

Alisema wanachama watakaofanikiwa kwenye programu hiyo inayoendeshwa kuanzia miezi mitatu, sita au mwaka 

mzima watafaidika kwa kujiongezea upeo wa mambo mbalimbali.
 Timu ya soka ya wanawake mkoani Lindi wakitambulishwa katika hafla hiyo. Nao wanatarajia kujiunga na Girl Guides.
 Mkufunzi Mkuu kutoka TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, Emmiliana Stanslaus akitambulishwa wakati wa hafla hiyo.
 Young Leader wa Dar es Salaam, Valentina Gonza akitambulishwa wakati wa hafla hiyo
 Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akijitambulisha.
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth Namatanga akimvisha beji mwanachama mpya.
 Mgeni rasmi, RPC Mzinga akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides.
 Makamu Mwenyekiti wa TGGA Lindi, Sharifa Mkwango akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides.
  Mkufunzi Mkuu wa TGGA, Emmiliana Stanslaus akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides.
 Girl Guides mpya akivishwa beji.
 Mkufunzi Msaidizi wa TGGA Mkoa wa Lindi, Kidawa Naheka akimvisha beji mwanachama mpya wa TGGA.
 Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi akimvisha beji mwanachama mpya.
 Katibu wa TGGA Mkoa wa Lindi  akimvisha beji mwanachama mpya.
 Girl Guides wapya wakila kiapo.
 Girl Guides mpya Elvila Dickson akisoma risala.
 RPC Mzinga akihutubia wakati wa hafla hiyo.
 RPC Mzinga akiwa na baadhi ya viongozi wa TGGA.
 RPC Mzinga akiwa na baadhi ya Girl Guide wapya pamoja na viongozi.

No comments:

Post a Comment

Pages