Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (R)amekutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq
Pardesi (c) ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia
msimu ujao.(L) Ni Meneja wa Namera Bwana Muhammad Waseem. Waziri Mkuu amekutana
nao leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
*Aahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini
*Aahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw.
Hamza Rafiq Pardesi ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini
kuanzia msimu ujao.
Amekutana na Bw. Pardesi leo (Jumanne, Septemba 12, 2017)
kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam na amesema
kwamba tayari Serikali imeanza kuwahamasiha wakulima kuongeza uzalishaji kwa
kuwa kuna soko la uhakika.
Waziri
Mkuu amempongeza Bw. Pardesi kwa kuiunga mkono Serikali katika mpango wake wa
kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda. Kampuni ya Namera Group of Industries
inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya jijini Dar es Salaam.Kampuni
inatarajia kufungua kiwanda kingine cha nguo wilayani Kahama.
Pia Waziri
Mkuu amesema katika kuhakikisha zao la pamba linapewa kipaumbe alikutana na
wakuu wa mikoa yote inayolima pamba Ijumaa, Septemba 8, 2017 na aliwaagiza
wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato
wananchi hususan wakulima wa zao la pamba.
Amesema
Serikali imeamua kufufua mazao makuu matano ya biashara ambayo ni pamba, chai,
kahawa, korosho na tumbaku ili kuwawezesha wakulima kupata tija na kuondokana
na umasikini wa kipato, hivyo kukuza uchumi wa Taifa.
Waziri
Mkuu amesema Serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba kuanzia maandalizi ya
shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko, hivyo
ahadi yao ya kununua pamba yote ni faraja kwa wakulima.
“Nimefurahishwa
na uamuzi wenu wa kutaka kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia
msimu ujao kwani kwetu sisi ni faraja kwa sababu wakulima walipunguza
uzalishaji baada ya kukosa soko la uhakika.”
Kwa upande wake Bw. Pardesi amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba
kampuni yao inauwezo wa kununua pamba yote inayozalishwa nchini na kuichakata
katika viwanda vyao na kutengeneza nguo zitakazouzwa nchini kwa bei nafuu.
Amesema kwa sasa wameajiri mafundi katika viwanda vyao
ambao watakuwa wa nashona nguo na kuziuza nchini kwa gharama nafuu ili
kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kumudu kununua na kuondokana matumizi ya
nguo za mitumba.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi Namera tuko tayari kununua
pamba yote inayozalishwa nchini kwani viwanda vyetu vinafanya kazi ya kuchambua
pamba, kutengeneza nyuzi na majora kisha tunashona nguo na kuziuza. Hapa Kazi
Tu maana bila ya kufanya kazi huwezi kuheshimika.”
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kitendo cha kununua
pamba inayolimwa nchini na kuchakata katika viwanda vyao kwa lengo la
kutengeneza nguo za aina mbalimbali wataiwezesha Serikali kuokoa fedha nyingi za
kigeni zilizokuwa zinatumika kuagiza nguo nje ya nchi.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE,
SEPTEMBA 12, 2017.
No comments:
Post a Comment