NA TATU MOHAMED
RAIS na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk.
Ally Mohammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mkutano na
utoaji wa Tuzo za Pan African Humanitarian Summit.
Mkutano na utoji wa Tuzo hizo zenye lengo la kutambua
jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau barani Afrika ili kuendeleza
na kudumisha diplomasia na amani utafanyika Novemba 18 mwaka huu jijini
Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
jana, Mratibu wa mkutano huo kutoka Asasi ya Vijana wa umoja wa Mataifa
(YUNA), Selemani Kitenge, amesema mkutano huo utatoa fursa kwa watu
mbalimbali wakiwamo Watu mashuhuri kutoka nchi tofauti barani Afrika
kujadili mustakabali wa diplomasia na amani.
"Kwa upande wa tuzo pamoja na vipengele vingi lakini kuna
viwili muhimu ambavyo ni pamoja na cha Rafiki wa Afrika ambacho ni
mahsusi watu walio nje ya Afrika ambao wamekuwa mchango mkubwa katika
masuala mbalimbali barani hapa.
"Kipengele cha pili ni Peace Building (Mlinda amani) tuzo
ambayo itatolewa watu ambao wamefanya vizuri katika kuhamasisha amani na
diplomasia," amesema.
Ameongeza kuwa mkutano huo utawaleta pamoja wanadiplomasia,
wadau wa maendeleo pamoja na vijana madhubuti kutokana katika nyaja
mbalimbali barani Afrika,viongozi wa serikali.
Kitenge amesema dhima ya mkutano huo kwa mwaka huu ni Amani inawezekana Jana,sasa na kesho.
Aidha amesema tuzo hizo zilianza kutolewa toka mwaka 2015 ambapo Tanzania ni nchi ya pili kuandaa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment