Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano UTT AMIS, Daudi Mbaga, akitoa elimu ya Uwekezaji wa Pamoja wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Maaskofu uliofanyika Kurasini jijini Dar es Salaam huku ukiwa na lengo la kujadili uendelezaji wa utoaji huduma bora za elimu na afya zinazotolewa na makanisa nchini na kudhamini na UTT AMIS.
Rais wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), Askofu Dkt. Fredrick Shoo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa mkutano wa siku mbili wa CSSC uliowashirikisha Maaskofu 150 huku ukiwa na lengo la kujadili uendelezaji wa utoaji huduma bora za elimu na afya zinazotolewa na makanisa hapa nchini.
Baadhi ya maaskofu wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Malasusa, akifuatilia mkutano huo.
No comments:
Post a Comment