HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 10, 2017

HAKUNA MGOMO WA MABASI-CHAKUA

Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Hassan Mchanjama (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari. (Picha ya Maktaba).

Na Shehe Semtawa

MWENYEKITI wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Hassan Mchanjama, amewataka Watanzania kupuuza tamko lilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Enea Mrutu kwamba siku ya Jumapili kutakuwa na mgomo.


Mchanjama, aliyasema hayo baada ya abiria na baadhi ya vyombo vya habari kupiga simu kutwa nzima ya leo, katika ofisi za Chakua wakiuliza kama mgomo huo utakuepo kweli kama ulivyotangazwa na Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), juzi.



Kwa mujibu wa taarifa ya Chakua, inawajulisha abiria na jamii kwa ujumla kwamba mgomo huo haupo kama ilivyopotosha na kikundi cha wanachama wachache wa (Taboa).


"Kwa taarifa hii Chakua Makao Makuu jijini Dar es Salaam, inawataka na kuwatoa hofu abiria kuwa waendelee na ratiba zao za safari kama kawaida kwa ajili ya masilahi yao binafsi na taifa kwa ujumla," alisema Mchanjama.


Aidha, Mchanjama ameiomba jamii kuipuuza taarifa hiyo iliyotolewa na Taboa kwa sababu katika chama hicho wapo baadhi ya wamiliki waadilifu ambao hawako tayari kuingia kwenye migogoro na serikali.


"Uzoefu unaonyesha Taboa huwa wanataka tu kujitafutia umaarufu kupitia kutangaza migomo kupitia vyombo vya habari tukumbuke hii sio mara ya kwanza kwa kikundi hiki na wafuasi wake kutangaza migomo kwenye vyombo vya habari lakini haifanikiwi


"Hii ni kwa vile wamiliki wenyewe hasa wa mabasi ya abiria huwa hawaitii matangazo ya Taboa kutokana na hali hiyo abiria tuendelee kupanga safari na kusafiri kama kawaida popote tutakapo kama sheria inavyoturuhusu," alisema Mchanjama ambaye ni Mwenyekiti Taifa Chakua na Msemaji Mkuu wa chama hicho Tanzania.


Mchanjama, alisema licha ya vikwazo inavyopambana navyo kutoka kwa mafisadi bado Chakua itaendelea kupigania utekelezwaji sheria zinazolinda haki za abiria usiku na mchana hadi pale watoa huduma wakaidi watakaponyooka.


Mwenyekiti wa Taboa, juzi alikaririwa na vyombo vya habari akisema siku ya Jumapili watafanya mgomo kupinga kitendo cha Mamlaka ya udhibit wa usafiri wa majini na nchi kavu (Sumatra), kupuuza maoni yao ambayo walitaka yawe SHERIA.


Aliyataja maoni hayo kuwa ni Taboa kutaka kutenganishwa makosa ya dereva na mmiliki pia faini ya sh. 200,000 ipunguzwe kwani ni kubwa mno.

No comments:

Post a Comment

Pages