HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 11, 2018

Serengeti Lite mdhamini rasmi Ligi ya soka la Wanawake


Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie na Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya wanawake kupitia chapa ya Serengeti Premium lite ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Ofisa mkuu wa michezo wa wizara ya habari, utamaduni,sanaa na michezo Henry Lihaya (katikati waliosimama) akishuhudia tukio la kusaini Mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya Wanawake kupitia kampuni ya Serengeti Breweries Ltd.Mkataba huo umesainiwa kati ya SBL (Mkurugenzi Mtendaji wake ni Helene Weesie) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF (,Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura).Ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu .

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie na Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya wanawake kupitia chapa ya Serengeti Premium lite ambapo SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Dar es Salaam, Januari 10 2018: Bia pendwa ya Serengeti Premium Lite, ambayo inazalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), leo imetangaza kuwa mdhamini rasmi wa Ligi ya Taifa ya Soka la Wanawake (Women Premier League). Katika Mkataba uliosainiwa kati ya SBL na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), SBL itatoa jumla ya shilingi milioni mia nne na hamsini (TZS 450m) ili kuzidhamini timu zote zinazoshiriki katika ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Kama mdhamini rasmi wa ligi hiyo, Serengeti Premium Lite itatoa msukumo kwa timu zote nane za wanawake kwenye ligi ambapo mshindi atakuwa mwakilishi wa taifa katika mashindano ya kikanda na ya kimataifa. Kupitia udhamini huo, SBL ina matumaini makubwa kwamba itaweza kuwazindua wananchi na hasa mashabiki wa soka na kuwaunganisha pamoja ili kuongeza hamasa katika ligi ya taifa ya wanawake kupitia bia hiyo kipenzi cha watanzania ya Serengeti Premium Lite.

“Tunayo furaha kubwa kuwa wadhamini rasmi wa Ligi ya Taifa ya Soka la Wanawake kupitia bia yetu maarufu ya Serengeti Lite. Siku zote tumekuwa tukiamini katika kuendeleza vipaji katika sehemu mbali mbali za nchi na haswa inapokuja katika michezo inayotuleta pamoja. Tunaamini udhamini wetu utawavutia mashabiki wa rika mbali mbali kuiunga mkono ligi ya wanawake na kufikia mafanikio makubwa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, SBL inaamini katika nguvu ya mpiga wa miguu ambayo inawaunganisha watu.

Udhamini wa Twiga Stars unafuatia historia ndefu ya udhamini wa timu ya soko ya wanaume, Taifa Stars ambayo mpaka hivi sasa inaendelea kupata udhamini wa SBL kupitia bia yake mama ya Serengeti Premium Lager. SBL ni sehemu ya kampuni ya Diageo ambayo inauhusiano mkubwa na masuala ya soka duniani ikiwa ni pamoja na udhamini wa Ligi Kuu ya Uingereza kupitia bia ya Guinness

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura alisema; “Leo kwa mara nyingine tunashuhudia ushikiano muhimu kati yetu na SBL, kampuni maarufu ya bia na ambayo imekuwa mstari wa mbele kwa kusaidia maendeleo ya michezo nchini. Ushirikiano huu utasaidia sana katika kuendeleza soka letu la wanawake pamoja na mashindano tutakayokuwa tunaandaa. Tunafurahia udhamini huu kupitia bia ya Serengeti Lite na tunaamini utakuwa wa mafanikio makubwa,”

Utiaji saini kati ya pande hizo mbili ulishuhudiwa na Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Bw, Yusuph Singo ambaye aliipongeza SBL kwa kujitolea kwake katika kuunga mkono sekta ya michezo nchini na pia kuwataka Watanzania wenye mapenzi mema pamoja na makampuni mengine kuiga mfano mzuri wa kampuni ya SBL.

No comments:

Post a Comment

Pages