Na Mwandishi Wetu, JWTZ
Wapiga golf 12 akiwemo aliyekuwa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi jenerali Mstaafu George Waitara wameanza vyema mwaka kwa kuibuka washindi katika michuano ya Golf inayofanyika kila baadaya Miezi Mitatu ambapo kwa mwaka 2018 ndio ya kwanza.
Katika mashindano hayo yaliyokuwa na msisimko na kushirikisha wacheza golf 73 kutoka katika makundi matano ambayo ni Watoto(Juniors), Seniors, Wanawake Divisheni A, B na C huku idadi kubwa ya wanawake wakiendelea kujitokeza.
Katika kundi la Divisheni A Mshindi aliiibuka Seif Mcharo ambaye ni miongoni mwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Golf baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 71 akifuatiwa na Kapteni Kibuna Shaabani aliyepata Mikwaju ya Jumla 74 huku Divisheni B Mshindi akiibuka Likuli Juma Baada ya Kupata mikwaju ya Jumla 70 akifuatiwa na Michael Lotich aliyepiga 74.
Kwa Upande wa Kundi C Sajini Taji John Msey aliibuka mshindi baada ya kupata Mikwaju ya Jumla 76 akifiuatiwa na Balozi Sai Kapale aliyepiga mikwaju ya Jumla 81 wakati katika kundi la wanawake Habiba Juma aliibuka Mshindi na kueneleza historia ya yake ya kufanya vyema baada ya kupiga mikwaju ya jumla 76 na kumshinda Mwenzie Lilian Mwaulambo kwa Count Back baada ya kufungana kwa Mikwaju 76.
Katika kundi la Senior Jenerali Mstaafu George Waitara alibuka mshindi Baada ya kupata net ya 72 akifuatiwa na Brigedia Jenerali Mstaafu Julius Mbilinyi aliyepata Net ya 76 huku katika kundi la Watoto Zabron Hamis aliibuka mshindi kwa mikwaju ya jumla 70 na kufuatiwa na Karimu Ismail aliyepiga 74.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema ni mashindano ya kwanza kwa mwaka 2018 lakini yameweza kuitoa Dira ya mwelekeo wa Wachezaji.
Pia aliahidi kuendelea kuwekeza katika kuibua Wachezaji wapya na kuendeleza waliopo ikiwemo kuhakikisha wanashiriki Michuano mbalimbali ya Kimataifa na Kitaifa na kiletea heshma nchi na klabu ya jeshi ya Lugalo.
Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo aliwataka wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuwa wanachama wenye nidhamu kama ilivyo ada ili kufanikiwa kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment