Mkuu wa wilaya ya Chemba ,Simon Odunga akifafanuajamba wakati kamati ya maafa ya wilaya nakata ya Mrijo walipokutana na wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajiliya tahmini ya athari zamaafa ya mafuriko katika katika wilaya hiyo.
Baadhi ya nyumba ambazo zimezungukwa na maji katika kata ya Mrijo wilayani Chemba kutokana na maafa ya mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyenya wilayani humo.
Na Mwandishi Maalum
Baadhi ya nyumba ambazo zimezungukwa na maji katika kata ya Mrijo wilayani Chemba kutokana na maafa ya mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyenya wilayani humo.
Na Mwandishi Maalum
SERIKALI
wilayani Chemba mkoani Dodoma imesema kuwa imepanga kuwahamisha watu wanaoishi
maeneo hatarishi ya kupata mafuriko kutokana zaidi ya kaya 2,000 zimezungukwa
na maji katika kata ya Mrijo hadi hivi sasa.
Akiongea
wakati akitoa taarifa kwa waratibu wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu
waliokwenda kufanya tathimini ya maafa yaliyotokana na mafuriko ya mvua
zinazoendelea kunyesha wilayani humo, mkuu wa wilaya ya Chemba, Simon Odunga alibainisha
kuwa mkakati wa muda mrefu walionao ni kuwatafutia wakazi hao maeneo
salama.
Odunga
Alisema kuwa kwa sasa kamati za maafa zimechukua hatua ya kukabili maafa ya
mafuriko kutokana na idadi ya nyumba
zilizozungukwa na maji imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha hivyo wameanzisha kambi maalum kwa watu ambao nyumba zao
zimeanguka kutokana na maafa hayo.
Aliongeza kuwa msaada wa haraka
unahitajika kutokana na waathirika hao wa mafuriko kutumia baadhi ya majengo ya madarasa ambayo yanapaswa
kutumiwa na wanafunzi ambao wanajiunga
na masomo mwaka huu.
“kwa
sasa tunahitaji sana mahema, mataulo, mashuka , chakula pamoja na madawa
kwajili ya kuwahudumia hawa watu ambao tunao hapa na tukipata vifaa hivyo basi
tutaondoka hapa na kwenda kutengeza kambi sehemu nyingine ambayo tumeiandaa
maaluum kwajili ya kuwahifadhi hawa watu na kuacha haya madarasa kwajili ya
matumizi ya wanafunzi” alisema Odunga.
Mkuu
huyo wa wilaya aliongeza kuwa tayari wilaya imeshaunda kamati mbalimbali ambazo
zinahusika katika kusaidia wahanga hao kuwa salama kiafya kwa kuchukua
tahadhari zinazoweza kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko.
Naye
mratibu wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu Ally Mwatima, alisema kuwa
mahitaji yote ambayo yameanishwa na mkuu huyo wa wilaya wameyachukua na
watayawasilisha ili hatua ziweze kuchukuliwa mapema iwezekanavyo.
“Kwanza
niwapongeze kwa kukabili maafa kwa mujibuwa sheria,kanuni namiongozo ya
menejimentiya maafa, hali hii imesaidia
kuokoa maisha ya hawa wenzetu na mahitaji yote mliyobainisha ni ya msingi sana
hivyo tutakwenda kuonana pia na kamati ya maafa mkoa ili kuweza kuona na sisi
tunaongeza nguvu katika vitu gani vya msingi ambavyo vitawasadia hawa
wenzetu”alisema Mwatima.
No comments:
Post a Comment