HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2018

DStv yawasha moto wa kombe la Dunia 2018!


  Watangazaji Nguli Kurindima kwa Kiswahili
Wateja kutazama popote walipo
 Mtanange huo kuonyeshwa live kwenye vifurushi vyote 
Channel maalum 6 kuonyesha Michuano hiyo katika HD
Dar es Salaam, Tanzania
 Huku zikiwa zimebaki siku chache kwa kinyang’anyiro cha Kombe la Dunia  2018 kuanza nchini Urusi, Kampuni ya MultiChoice Tanzania imetangaza neema kwa Watanzania kwa kutoa ofa maalum kwa wateja wapya, huku ikitenga chaneli 6 maalum zitakazoonyesha michuano hiyo katika kiwango cha HD pamoja na kuwawezesha wateja wake wote kufuatilia michuano hiyo kwa Lugha ya Kiswahili katika vifurushi vyote vya DStv.
“Hii ni zaidi ya ofa” anasema Ronald Shelukindo, Mkuu wa Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania wakati akitangaza ofa hiyo jijini Dar es Salaam jana. “Sasa tunataka watanzania waweze kupata burudani ya kombe la dunia 2018 kwa namna tofauti kabisa. Kwanza kwa wateja wapya wataweza kujiunga kw shilingi 79,000 tu na kupata seti ya DStv pamoja na kifurushi cha miezi miwili bure!” alisema Shelukindo na kuongeza “Kama hiyo haitoshi, wateja wote wa DStv, sasa wataweza kupokea matangazo ya moja kwa moja kwa lugha ya Kiswahili ambapo tuna timu ya watangazaji mahiri wa soka hapa nchini watakaowaletea watanzania burudani hii”
Amesema mbali na ofa hiyo na kutangazwa kwa michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili, pia DStv imetenga chaneli 6 mahususi kabisa kwa ajili ya michuano hiyo pamoja na kuhakikisha kuwa wateja wanaweza kutazama DStv popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu, laptop na tablet. “Hivi sasa ukipakua app yetu ya DStv Now, unaweza kutumia hadi vifaa vitano tofauti ambavyo vyote huunganishwa na dikoda yako hivyo kuwawezesha wanafamilia kutazama vipindi tofauti kwa wakati mmoja” alisema Shelukindo.
Akitoa maelezo kuhusu jinsi DStv ilivyojizatiti kuwahakikishia watanzania burudani isiyo na kifani msimu huu wa kombe la dunia, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria, amebainisha kuwa DStv itaonyesha michuano hiyo katika vifurushi vyake vyote, hivyo wateja wote wa DStv watafurahia michuano hiyo tena katika muonekano angavu yanni HD.
“Kwakeli msimu huu wa kombe la Dunia, kila atakayekuwa na DStv atakuwa anapata hasa kile anachostahili kwani mechi zote zitaonekana live, kwenye HD na kwenye vifurushi vyote, huku pia zikitangazwa kwa lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili” alisema Alpha
Amesema kwa wale wanaotaka kufuatilia kwa Kiingereza wataweza kuona kupitia DStv, wale wa Kireno wataona kupitia DStv, wale wa Kifaransa pia wataona kupitia DStv, na kikubwa zaid sisi watanzania tutaweza kufuatilia kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili kupitia DStv. “Tumejipanga, kuwapa watanzania burudani ya aina yake msimu huu wa kombe la Dunia” Alisisitiza Alpha.
Katika uzinduzi huo, DStv iliwatambulisha rasmi watangazaji wa soka ambao watakuwa wakiwaletea watanzania matangazo hayo kwa Kiswahili ambapo majina makubwa ya watangazaji na wachambuzi wa soka yamo.
 Waliotambulishwa ni Aboubakary Liongo, Maulid Kitenge, Ephaim Kibonde, Edo Kumwembe, Ibrahim Masoud - Maestro na Oscar Oscar.
Wakiongea baada ya kutambulishwa, watangazaji na wachambuzi hao mahiri wa soka wamesema wamejizatiti kikamilifu kuhakikisha kuwa wanawaletea matangazo na uchambuzi wa kina ili kuhakikisha kuwa kila mpenda soka anafurahia na kuyaelewa vizuri mashindano hayo.
“Mwaka huu mtoto hatumwi sokoni. Kwa DStv, hii ni zaidi ya kombe la Dunia kwani tutakuwa tukiwaletea uchambuzi wa kina kabla, wakati na baada ya mechi. Bila shaka itakuwa ni burudani mwanzo mwisho” alikaririwa Maulid Kitenge, mmoja kati ya watangazaji hao.
Uzinduzi huo ulihudhuria na mamia ya wadau mbalimbali wa soka nchini wakiwemo wachezaji maarufu waliochezea timu mbalimbali pamoja na timu ya Taifa pamoja ni viongozi mbalimbali na wapenzi wa soka maarufu nchini. Pia wachezaji kadhaa wa klabu za Simba na Yanga walihudhuria hafla hiyo iliyokuwa ya kufana sana

No comments:

Post a Comment

Pages