HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 16, 2018

MKUTANO MKUU WA WANAHISA WA BENKI YA CRDB-AICC ARUSHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkuu wa 23 wa wanahisa wa benki hiyo unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha, Mei 19. Kulia ni  Mkurugenzi wa Mikopo, James Mabula.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkuu wa 23 wa wanahisa wa benki hiyo unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha, Mei 19. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko, Jadi Ngwale na Mkurugenzi wa Mikopo, James Mabula.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkuu wa 23 wa wanahisa wa benki hiyo unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha, Mei 19. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko, Jadi Ngwale na Mkurugenzi wa Mikopo, James Mabula.

NA GRACE MACHA, ARUSHA

BENKI ya CRDB imepata faida ya shilingi 36 bilioni kwa mwaka uliopita licha ya kuwepo na changamoto nyingi za mabadiliko ya kiuchumi wa dunia ambayo iliwalazimu kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili mikopo inayoweza kuchechefuka. (mikopo ambayo inaweza isilipwe kwa wakati)

Hayo yameelezwa jana Mkurugenzi wa benki hiyo, Dk Charles Kimei wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya mkutano wao mkuu wa 22 wa wanahisa wa benki hiyo unaotarajiwa kufanyika keshokutwa (jumamosi) jijini hapa.

Alisema kuwa kabla ya kulipa kodi faida hiyo ilikuwa shilingi 53 bilioni ambapo alisema kuwa kilichoathiri faida yao kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita ni kwa benki kulazimika kutenga fedha nyingi kiasi cha shilingi bilioni 153  kwa ajili ya mikopo ambayo imechechefuka.

"Kwa kifupi niseme mwaka jana  benki yetu imefanya vizuri kulikuwa na changamoto nyingi lakini benki yetu imefanya vizuri kuliko tulivyotarajia. Tumepata faida ya shilingi bilioni 36 ni ndogo kulingana na jinsi ambavyo tulikuwa tunapata  lakini changamoto tulizokumbana nazo ni nyingi sana na tumeiweka benki mahali pazuri kwa kupata faida mara mbili zaidi katika kipindi cha mwaka huu na miaka inayofuata," alisem Dk Kimei na kuongeza.

"Mikopo ndiyo imekula tengo kubwa sana ya fedha zetu. Ukifanya tengo kubwa haimaanishi umepata hasara zile fedha zinakaa kwenye 'reserve' ambayo inakaa kwenye 'balance sheet' kama akiba kwa ajili ya kuweza kupambana na matukio yanayokuja kwa hiyo ni fedha ambayo tunayo iko kwenye akaunti zetu lakini tumetenga nje ya faida ambayo tunaweza kuigawa kwa wanahisa wetu," alifafanua mkurugenzi huyo na kuongeza.

"Tulitenga shilingi bilioni153 kwa ajili ya mikopo hiyo kwa hiyo tusingeitenga tungepata faida ya zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa hiyo benki imefanya vizuri. Lakini kwa sababu ni benki ambayo tunaamini kwenye "sustainability' na kuendelea kutoa faida kwa miaka mingi ijayo tumeona kwamba ni vizuri tufanye tengo kubwa mwaka huu wa 2017,".

Mkutano huo wa wanahisa utatanguliwa na semina ya siku moja kwa wanahisa hao ambapo miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni uchumi , uwekezaji wa kwenye hisa na namna ya kuridhisha hisa kwa wapendwa wao au watoto pindi mwanahisa atakapofariki.

"Kutakuwa na majadiliano kuhusiana na  uchumi wa ulimwengu kwa ujumla na mambo gani yanajitokeza kwenye uchumi huo na kubadilisha mwenendo wa mabenki kwa ujumla.Hasa kwenye mambo ya viwango vya ukaguzi wa mahesabu ya mabenki na  utunzaji wa fedha za benki viwango vya kimataifa vimebadilika sana," alisema Dk Kimei na kuongeza.

"Tunapenda kuwaelimisha anahisa wetu kwasababu tunajua si watawekeza kwetu tu kwenye hisa zetu lakini wanaweza wakanufaika kwa benki yao kuwapa elimu juu ya namna gani wanaweza kutunza hisa walizowekeza hata kwenye makampuni mengine,".

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na wanahisa zaidi ya 1,500.

No comments:

Post a Comment

Pages