NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Hifadhi za Jamii (NSSF), limesema lipo kwenye hatua za mwisho za uhakiki wa madai ya waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni za Pan Africa na Pangae kabla ya kuanza kuwalipa juma lijalo.
Wafanyakazi zaidi ya 2,000 wa kampuni hizo waliachishwa kazi Oktoba mwaka 2017 kwenye mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi, uliopo Kahama mkoani Shinyanga.
Kuachishwa kazi kwa wafanyakazi hao kuliwalazimu kuomba kulipwa mafao yao jambo lililokuwa likifanyiwa uhakiki na shirika hilo ili kubaini uhalali wa malipo hayo kabla hayajafanyika.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bathow Mmuni alisema uhakiki wa madai hayo makubwa upo kwenye hatua za mwisho hivyo amewataka wafanyakazi hao kujiandaa kupokea mafao yao.
“Shirika linatumia nafasi hii kugaganua kwamba madai yote ya wanachama hao yanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu na ni haki yao pia, yakishadhibitishwa yatalipwa mara moja.
“...haya ni madai ya fedha nyingi lazima tujiridhishe ili kila mchangiaji alipwe stahiki zake kwa usahihi… wasiwe na wasiwasi shirika letu linazo fedha za kutosha kujiendesha na kutimiza majukumu yake yote ikiwemo kulipa mafao,” alisisitiza Mmuni na kubainisha kwmaba wataanza kulipwa kuanzia juma lijalo.
No comments:
Post a Comment