Msimu wa Ligi wa 2017/2018 kwa mujibu wa Kalenda ya Mashindano ya
Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF).
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambao ndiyo waendeshaji wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL)
tunatoa pongezi kwa timu ambazo zimefanikiwa kupanda daraja.
Kwa
upande wa FDL zilizopanda kwenda VPL msimu wa 2018/2019 kulingana na
msimamo wa mwisho wa Ligi hiyo ni; Kundi A ni JKT Tanzania FC ya Dar es
Salaam na African Lyon ya Dar es Salaam.
Kundi B
ni Kinondoni Municipal Council FC ya Dar es Salaam na Coastal Union ya
Tanga wakati Kundi C ni Biashara United FC ya Musoma na Alliance Schools
FC ya Mwanza.
Kwa upande wa SDL zilizopanda
kwenda FDL msimu wa 2018/2019 ni timu nne zilizoongoza makundi pamoja na
washindwa bora (best looser) watatu. Kundi A ni Reha FC ya Dar es
Salaam, Kundi B ni Arusha FC ya Arusha, Green Warriors ya Dar es Salaam,
na Mashujaa FC ya Kigoma.
Washindwa bora ni Namungo FC ya Lindi, Pepsi FC ya Dar es Salaam, na Boma FC ya Kyela, Mbeya.
IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment