Mkurugenzi Mkuu wa Tazama, Davison Thawethe, akizungumza katika hafla ya utoaji wa gawio la Sh. Mil. 681.8 kwa serikali ya Tanzania.
Wafanyakazi wa Tazama wakiwa katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa Nishati wa Zambia na Mwenyekiti wa Bodi ya Tazama,
Brigedia Emeldah Chola, akizungumza kabla ya kukabidhi gawio la Sh. Mil. 681.8 kwa serikali ya Tanzania.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani, akizungumza kabla ya kupokea gawio la Sh. Mil. 681.8 kutoka Tazama.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto),
akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Mil. 681.8 kutoka kwa
Katibu Mkuu wa Nishati wa Zambia na Mwenyekiti wa Bodi ya Tazama,
Brigedia Emeldah Chola (wa pili kulia), ikiwa ni gawio kwa Tanzania
kutoka Tazama, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
BOMBA la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Dar es
Salaam hadi Ndola Zambia, linalomilikiwa na
Tanzania na Zambia (Tazama), limetoa gawio la Sh. milioni 681.8 kwa
Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani alisema
hii ni mara ya kwanza kwa bomba hilo kutoa gawio kwa wanahisa wake tangu
kuanzishwa miaka 50 iliyopita.
Alisema kutotolewa kwa gawio kulitokana na bomba
hilo kufanya kazi kama watoaji huduma jambo lililofanya washindwe kutengeneza
faida na badala yake kujiendesha kwa hasara.
“Hili ni tukio la kihistoria tumefanya kazi kwa
miaka 50 hatujawahi kupata gawio lolote, awali shirika lilikuwa linafanya kazi
kama watoa huduma kwa nchi hizi katika kusafirisha mafuta lakini kuanzia mwaka
jana mfumo umebadilika na sasa linafanya kazi kibiashara” alisema Amina.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Nishati wa Zambia na
Mwenyekiti wa Bodi ya Tazama, Brigedia Emeldah Chola alisema kwa mwaka jana
waliingiza Bilioni 11.4 ambapo wametoa Sh. bilioni 2.0 sawa na asilimia 20 ya
mapato yake kwa wanahisa.
Alisema katika gawio hilo Zambia ambayo wanamiliki
2/3 ya hisa wamepata Sh.bilioni 1.2.
“Gawio linaonekana kuwa dogo lakini kwangu naona ni
hatua muhimu kwani ni inaashiria kutoka kwenye kupata hasara kutokana na
kufanya kazi kwa mazoea” alisema Chola.
Alisema wamedhamiria kuongeza ufanisi katika
utendaji kazi pamoja na kuongeza
mikakati itakayosaidia kuongeza thamani kwa wanahisa wao kwa kuzingatia
miongozo ya serikali.
Aidha alitaja baadhi ya mikakti waliojiwekea kuwa ni
pamoja na kuongeza upana wa bomba hilo lenye ukubwa wa Kilomita 914 kufikia
inchi 12 kutoka nane za sasa mradi utakoagharimu Dola za Marekani milioni 350
na kuongeza kuwa baada ya kufanya hivyo bomba hilo litakuwa na uwezo wa
kusafirisha Tani milioni 1.5 kwa mwaka.
Jingine ni
kujenga bomba jipya kwa ajili ya mafuta yaliyokwishachakatwa ambao unatarajiwa
kugharimu Dola za Marekani Bilioni 1.5 pamoja na kuwa na utaratibu wa kukagua
mitambo yao mara kwa mara ili kuweza kufanya maboresho kabla ya kuchakaa na
kuhitaji mataengenezo makubwa.
No comments:
Post a Comment