HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 25, 2018

TCRA WATOA LESENI KWA WATOA HUDUMA ZA HABARI MTANDAONI


Mkurugenzi TCRA asema 45 ndio wamekidhi vigezo kati ya waombaji 262*Asema mchakato bado unaendelea, atoa sababu kuweke gharama za usajili

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema leo ni siku muhimu katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na kushuhudiwa wadau wa habari wakiwa wamekamilisha hatua za usajili ili watambulike na kutumia fursa hiyo ya utoaji na upashaji habari kupitia mtandao wa intanenti.

Kutokana na kukamilisha mchakato huo TCRA imetoa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao wa intanenti 45 kati ya watoa huduma 262 walioomba na kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa.Miongoni mwa waliopewa leseni baada ya kukamilisha taratibu hizo ni pamoja na Michuzi Media Group (MMG).

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba wakati akikabidhi cheti cha usajili kwa wamiliki 45 wa Blogs, Redio na televisheni za mtandaoni na kusema kuwa zipo faida nyingi za habari na utangazaji kwa njia ya mtandao ambazo zinafahamika kwa wengi.

"Kama tunavyofahamu kwa miongo mingi sasa sekta ya habari na utangazaji imekuwa ikipata habari kwa njia ya redio na televisheni kupitia majukwaa mbalimbali kama mitambo iliyojengwa ardhini,Satellite na Cable.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba, akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao , iliyofanyika leo  katika ukumbu wa TCRA jijini Dar es Salaam. Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Blogers, Krants Mwantepele akizungumza kuhusiana na mwitikio ulionyeshwa kwa wamiliki kujisajili TCRA iliyofanyika , jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group (MMG), Ainde Ndanshau katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mkurugenzi wa Blogu ya Wananchi, William Malecela ‘LE MUTUZ ‘ Vkatika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mwakilishi wa  Mtandao wa Bongo 5, Yassin Ng’itu katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA, jijini Dar es  Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mmiliki wa Habari Mseto , Francis Dande katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa  Mmiliki wa Radio Seven ya Mtandaoni,  Atu Mandoza katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam. Baadhi ya waandishi na wamiliki wa watoa huduma kwa njia ya mtandao

No comments:

Post a Comment

Pages