HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 25, 2018

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA SH. MILIONI 240 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA DHARULA HOSPITALI YA BUNGANDO, MWANZA

 Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka, akitoka hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Beki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, katika hafla ya kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shs. Mill 240 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ukarabati na upanuzi wa Jengo la Huduma za Wagonjwa wa Dharula katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bungando, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk. Abel Makubi. 
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (katikati), akikabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Beki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, mfano wa hundi yenye thamani ya Shs. Mill. 240 kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bungando, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ukarabati na upanuzi wa Jengo la Huduma za Wagonjwa wa Dharula (Emergency Medicine Department) katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Tully Mwambapa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dkt. Abel Makubi, akimueleza jambo Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (koti jeusi) pindi walipotembelea sehemu ya Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) inayofanyiwa ukarabati katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018. Wengine pichani ni baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB pamoja na Uongozi wa Hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages