HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 20, 2018

BENKI YA CRDB YASAINI MKATABA WA KUIWEZESHA KIMTAJI BENKI YA WANANCHI TANDAHIMBA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati), akisaini Mkataba wa kuiwezesha Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA) kimtaji katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA), Rajabu Mmunda. Wanaoshuhudia kulia ni Mwanasheria wa Benki ya CRDB, Firmat Tarimo, Meneja Mkuu wa Benki ya Wananchi Tandahimba, Mugwagi Steven (kushoto waliosimama) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kulia), akibadilishana hati na Mkwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA), Rajabu Mmunda, ya Mkataba wa kuiwezesha Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA) kimtaji katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Benki ya Wananchi Tandahimba, Mugwagi Steven, kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka na anayeshuhudia katikati ni Mwanasheria wa Benki hiyo, Mwanasheria wa Benki ya CRDB, Firmat Tarimo.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu Benki hiyo kuisaidia mtaji Benki ya Wananchi Tandahimba.
 Mkwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA), Rajabu Mmunda, akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akizungumza katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages