Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imetangaza kuboresha mfumo wake wa mauzo na usajili wa laini za simu na sasa watakaofanya hivyo ni mawakala waliothibitishwa.
Uamuzi
huo ni mkakati wa kudhibiti usajili na mauzo ya laini za simu za
Halotel ikiwa ni hatua ya kukabiliana na udukuzi au udanganyifu wowote
unaoenda kinyume na sheria za mawasiliano nchini.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Halotel,
Mhina Semwenda, amesema kampuni hiyo imepunguza idadi ya mauzo ya laini
za simu kwa mawakala, lakini pia mawakala watauziwa laini nyingine mpya
mara tu watakapokuwa wamemaliza mauzo ya laini za simu za awali pamoja
na kuthibitisha kuwa laini walizopewa zimesajiliwa kwa wateja kwa
kufuata taratibu zote za usajili zilizowekwa na mamlaka husika”.
“Tumeweka
mfumo thabiti wa kudhibiti uuzaji wa laini za simu na usajili kutoka
kwa mawakala wetu, hili pia limeambatana na uhakiki na usajili mpya wa
mawakala wote wanauoza laini za simu za Halotel. Alisema Mhina na
Kuongeza,
“Tumewekeza
kwenye teknolojia ya kisasa zaidi itakayogundua na kuzuia udukuzi wa
aina yoyote ya mifumo ya mawasiliano, Tunafanya haya yote ili kuongeza
ufanisi pamoja na kuwadhibiti watu wenye nia ovu ya kutumia miundombinu
ya mawasiliano kuvunja sheria” alisema Semwenda.
Alisisitiza
kuwa mara zote, kampuni hiyo inafuata kanuni na sheria zilizopo ndiyo
maana imekuwa ikiwekeza fedha nyingi ili kufikisha huduma bora kwa
Watanzania hivyo haipo tayari kushuhudia watu wenye niaovu wakiharibu
malengo mema yaliyopo.
“Uwekezaji
mkubwa uliofanywa kwa miaka miwili iliyopita nimatokeo ya ushirikiano
mwema baina ta Tanzania na Vietnam. Ni uhusiano huo uliochangia kukuza
biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili hivyo Halotel itaendelea
kuzingatia sheria na kanuni za nchi pamoja na kuendelea kuboresha na
kutoa huduma zenye gharama nafuu kwa Watanzania,” alisema Semwenda.
No comments:
Post a Comment