Klabu
ya Lugalo imedhihirisha ubora wao wa mchezo wa gofu hapa nchini baada
ya kushinda mashindano ya TANAPA Lugalo open yaliyomalizika jumapili
jioni kwenye viwanja vya Lugalo.
Mashindano
hayo ya Gofu ya TANAPA Lugalo open yalishirikisha wachezaji zaidi ya
150 kutoka vilabu vya Arusha Gymkhana,Moshi Gymkhana,TPC,Morogoro
Gymkhana na Lugalo club.
Ushindi
walioupata klabu ya Lugalo katika mashindano hayo ni wa kujivunia
,kwani katika mashindano yalifanyika mwezi uliopita kwenye viwanja vya
Moshi Gymkhana klabu ya Lugalo iliweza kushinda.
Katika mashindano ya TANAPA Lugalo open ilianza kwa mchezaji wa Taifa Godfrey Gwacha kupata ushindi wa jumla upande wa Gross.
Mchezaji
huyo aliweza kupata ushindi wa jumla baada ya kupiga mikwaju gross 149
ambapo siku ya kwanza mchezaji huyo aliweza kupata gross 76 na siku ya
pili akapata gross 73.
Nafasi ya pili ilichukuliwa tena na Richard Mtweve kutoka Lugalo aliyepiga mikwaju ya gross 152
Lugalo
tena iliweza kutamba upande wa neti baada ya Agrey John kupata ushindi
wa jumla kwa kupiga mikwaju ya neti 138,akifuatiwa na Anold Simoni
kutoka Dsm Gymkhana aliyepata neti 139.
Kwa
upande wa Division A mshindi alikuwa naodha wa klabu ya Lugalo shabani
Kibuna aliyeshinda kwa mikwaju ya neti 142 akifuatiwa Isiaka Daud pia
kutoka Lugalo aliyepata neti 143.
Upande
wa Division B mshindi alikuwa Gerald Gadiel kutoka Lugalo aliyeshinda
kwa mikwaju ya neti 139 akifuatiwa na Tiger Lee kutoka Lugalo aliyepata
neti 147.
Lugalo
ilizidi kunyanyasa tena kwenye mashindano hayo upande wa Division C
baada Magoti Fabiani kushinda kwa upigaji wa mikwaju ya neti 144
akifuatiwa na Ton H.D pia wa Lugalo aliyepata neti 145.
Upande
wa wanawake nafasi hiyo ilikwenda kwa Habiba Juma aliyeshinda kwa
mikwaju ya neti 147 akifuatiwa na Khadija Selemani aliyepata neti 149
wote kutoka Lugalo..
Kwa
upande wa upigaji mipira kwa karibu nafasi hiyo ilikwenda kwa Leo
Bashiri kutoka Lugalo,na upande wa upigaji wa mipira ya mbali kwa
wanawake nafasi hiyo ilikwenda kwa Neema Olomi kutoka Arusha Gymkhana
No comments:
Post a Comment