Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipozungumza katika futari aliyoiandaa kwenye viwanja
vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofuturisha kwenye
viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018. Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, John Mongella. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Aliyasema
hayo jana jioni (Jumamosi, Juni 9, 2018) alipozungumza na viongozi na
wananchi wa Mkoa wa Mwanza baada ya kushirikiana nao katika futari
aliyowaandalia. Shughuli hiyo ilihudhuriwa na waumini wa dini
mbalimbali.
Waziri
Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanaishi
kwa amani na utulivu, jambo litakalowawezesha kufanya shughuli zao
kikamilifu, hivyo wasikubali kuchonganishwa kwa misingi yoyote.
“Nawaasa
viongozi wa dini msikubali kutumia makundi mengine nje ya taasisi zenu
kwa ajili ya kuwazungumzia masuala yenu kwa sababu watawachonganisha na
Serikali ambayo haipo kwa ajili ya kugombana na taasisi yoyote,”
alisisitiza.
Waziri
Mkuu alisema jukumu kubwa la taasisi za kidini ni kuhakikisha
wanawalinda waumini wao pamoja na kuwaongoza kwa kuwapa mafundisho mema
yanayompendeza Mwenyezi Mungu, ambayo yatawawezesha kuishi kwa amani .
Alisema
misingi ya amani na utulivu ikiwa pamoja na mshikamano walionao
wananchi umesababisha Tanzania kupata heshima kubwa dunia kote, hivyo ni
vema kila mwananchi ahakikishe suala la kudumisha amani linapewa
kipaumbele.
Pia
Waziri Mkuu alisema amefurahi sana kujumuika na wananchi wa Mkoa wa
Mwanza katika futari hiyo, ambapo aliwapongeza kwa kukamilisha uundaji
wa kamani za amani kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella amlishukuru Waziri Mkuu kwa
ukarimu wake kwa kuwaalika wakazi wa Mwanza katika hafla hiyo, ambapo
alisema Mwanza ni kitovu cha amani kwa kanda ya Ziwa na nchi za Maziwa
Makuu. T
“Mwanza
tumejipanga na tunashirikiana na taasisi zote kwenye njanja zote , tupo
pamoja na tunashirikiana katika kuimarisha amani na utulivu.
Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kutuamini na
tunamuahidi tutafuata falsafa zake katika utendaji wetu,”.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza na Askofu wa
Kanisa la Charismatic Episcopal Church of Tanzania (CECT), Charles
Sekelwa alisema wao wanaiunga mkono Serikali katika kudumisha amani na
wataendelea kushirikiana nayo.
Alisema awali kulikuwa na changamoto ya matabaka ya kidini iliyobabisha na
kutoelewana baina ya waislamu na wakiristo, ambapo kamati yao ilifanya
kazi ya kuyasulisha na sasa hali ni shwari. “Matabaka ya kiimani
yameisha na watu wa dini zote wanashirikiana vizuri,”.
Askofu Sekelwa alisema wao kama viongozi wa pande hizo mbili hawawezi kukubali
kuona kunakuwa na matabaka ya kiimani miongoni mwa waumini, hivyo
watakikisha wanaendelea kuwafundisha waumini wao umuhimu wa amani.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson, Naibu Waziri waNchi,
OR – TAMISEMI, Joseph Kakunda, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali baadhi ya wananchi wa mkoa wa
Mwanza
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JUNI 10, 2018.
No comments:
Post a Comment