*Ni ya kwanza Afrika, inauwezo wa kutambua aina za madini na yalikotoka
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa ya na ya kwanza barani
Afrika yenye uwezo wa kupima na kutambua aina mbalimbali za madini.
Amesema
maabara hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya umiliki wa madini na
kudhibiti utoroshwaji wa madini mbalimbali kati ya nchi moja na
nyingine.
Maabara
hiyo imefunguliwa leo (Ijumaa, Juni 8, 2018) katika Kituo cha Madini na
Jiosayansi cha Afrika (AMGC) kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu amesema uzinduzi wa maabara hiyo utawezesha wataalamu kutambua
aina za madini na nchi yanakotoka, hivyo kuondoa migogoro ya umiliki
wake.
“Maabara
hii litatuweza kulinda madini yetu na kufanya biashara ya madini
vizuri. Pia hii ni fursa nzuri kwa nchi za Afrika kutumia maabara hii
kupima madini yao na kubaini yalikotoka,” amesema.
Hata
hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha
wanaziwesha nchi wanachama kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya
madini pindi zinapohitaji.
Pia
Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kusaidia katika
ununuzi wa vifaa vya maabara hiyo pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu
watakaoiendesha.
Waziri
Mkuu, pia ameiomba Serikali hiyo kutoa mafunzo hayo kwa Watanzania
wengi zaidi ili kuongeza idadi ya wataalamu wa kuendesha maabara hiyo.
Pia,
Waziri Mkuu amefungua Mkutano 38 wa Mawaziri wa Madini kutoka nchi
Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika katika kituo cha AMGC.
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii
vilivyopo nchini ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama
zilizosheheni wanyama wa aina mbalimbali pamoja na fukwe za bahari.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JUNI 8, 2018.
No comments:
Post a Comment