Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, akipokea Tuzo ya Benki Bora Tanzania 2018, kutoka Jarida la Euromoney la nchini Uingereza. Tuzo hiyo ni ya mwaka wa sita mfululizo kwa NMB kushinda miongoni mwa mabeki ya Tanzania. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA
MWANDISHI WETU
JARIDA
kongwe nchini Uingereza linalojihusisha na masuala ya utafiti wa kiuchumi na kibiashara
la Euromoney, limeitangaza Benki ya NMB, kuwa Benki Bora ya Mwaka nchini Tanzania,
ikiwa ni mwaka wa sita mfululizo.
Tuzo
hiyo iliyotolewa juzi jijini London, inaifanya NMB kuwa Benki Yenye Faida Zaidi
Tanzania, inatokana na uimara wa taasisi hiyo katika Sekta ya Fedha, ilikofanya
vema kupitia mabadiliko ya kimfumo yanayohusisha huduma za kidijitali.
Ikizungumzia
mafanikio hayo, Euromoney katika taarifa yae limesema NMB kuwa Benki Bora
Tanzania, kumezingatiwa vitu vingi, ikiwemo utoaji elimu za kifedha, mabadiliko
ya kimfumo katika fedha na kutanua fursa za jamii kutumia huduma za kifedha.
Taarifa
hiyo iliongeza kuwa uwekezaji wa NMB katika teknolojia, umeleta ufumbuzi wa
changamoto za kushughulikia mahitaji ya wateja kwa njia za kimtandao (mobile
banking), kadi za benki na mawakala wanaotoa huduma.
Akizungumzia
mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, amesema benki
yake inajisikia fahari na kujivunia ushindi wa khistoria waliouweka kwa kuibuka
washindi wa tuzo hiyo kwa miaka sita mfululizo.
Alibainisha
ya kwamba, wanapenda kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wao, ambao ndio
wanaowasukuma katika kuwabunia huduma bora na kwamba wanaichukua tuzo hiyo kama
chachu ya kuendelea kutanua huduma bora kwa jamii.
Bussemaker
alisisitiza kuwa, benki yake inajivunia uanzilishi wa mabadiliko ya kimfumo
kwenda dijitali, ambayo ni sehemu ya mchakato wao wa huduma bora kwa wateja na
kwamba tuzo hiyo ni matunda ya safari ya ushirikiano baina ya benki na wateja
wao.
No comments:
Post a Comment