HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2018

RAIS MAGUFULI AKABIDHI HATI ZA VIWANJA VYA MABALOZI, MASHIRIKA YA KIMATAIFA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Balozi wa Afrika Kusini nchini Mhe. Thamsangqa Dennis Mseleku hati ya kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018.
Mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa baada ya kupatiwa bila malipo na Rais Dkt John Magufuli hati za viwanja vya kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018.
Rais  wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Balozi wa Unigereza nchini Mhe. Sarah Cooke  hati ya kiwanja cha  kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wadogo wa nchi mbalimbali baada ya kuwakabidhi bila malipo hati za viwanja vya kujengea mjini Dodoma kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi wa nchi   mbalimbali pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa maara baada ya kuwakabidhi Hati za Viwanja vilivyopo Makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Balozi pamoja na Mashirika hayo ya kimataifa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu  mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 30, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Picha kutoka kwa Balozi mteule wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu. Zawadi hiyo ya picha imetoka kwa Mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Mama Ngina Kenyatta na katika picha hiyo anaonekana Rais Dkt. Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mama Ngina Kenya walipokuwa Nairobi nchini Kenya. Picha na IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages