Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania,
Allen Mushi (Kulia) akimkabidhi mfano wa
hundi mshindi wa droo ya Perfect 12, Ally Fundi kutoka Lindi aliyejishindia Sh 126.2 milllioni baada ya kubashiri matokeo
ya mechi 12 kwa usahihi. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Dar es
Salaam. Shabiki wa timu ya Simba na Barcelona ya Hispania, Ali Ahmad Fundi (40)
ameshinda Sh 126,241,620 baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa
kampuni ya M-Bet.
Fundi ambaye
ni mkazi wa Lindi alisema kuwa alibashiriki kwa kupitia simu yake ya mkononi na
kuibuka na kufanikiwa kushinda kiasi kikubwa hicho cha fedha.
Alisema kuwa
alipokea taarifa za ushindi kwa furaha sana kwani katika maisha yake,
hakutarajia kupata kiasi hicho cha fedha.
“Nimefarijika
sana, sikuamini kwani awali marafiki zangu walisema napoteza fedha, lakini
niliendelea kucheza baada ya kuona baadhi ya Watanzania wanshinda fedha nyingi
kupitia mchezo wa Perfect 12, niliamini siku moja nami nitakuwa mmoja wa
washindi,” alisema Fundi.
Alisema kuwa
ametumia Sh1,000 tu na kuibuka na kitita kikubwa cha fedha. “Kabla ya kushinda,
nilitumia nilibet mara tatu na kutumia Sh3,000, sikukata tamaa na leo kuibuka
na ushindi,” alisema Fundi.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi alisema kuwa kupitia ushindi huo,
serikali alijipatia kiasi cha fedha cha Sh25,248, 124 ikiwa kodi ya asilimia 20
kwa mujibu wa sheria.
Mushi
alisema kuwa mbali ya Fundi, pia kulikuwa na washindi 1,058 walioshinda kwa kubashiri kwa usahihi
mechi tisa, ambapo ambao walizawadiwa Sh1,854,630 huku washindi watu 175
waliweza kubashiri kwa usahihi mechi 10 na kuzawadiwa Sg sh2,472,840 na watu 11
waliweza kubashiri michezo 11 kwa usahihi na kuzawadiwa jumla ya Sh2,884,980.
“Kwa droo ya
840 pekee, tumeweza kutoa washindi 1,243 na kutumia fedha Sh133, 464,070
kuwazawadia washindi. Tunaomba Watanzania kuendelea kubeti kwa kutumia
michezo yetu na kufaidika kwa kuondoa umaskini,” alisema Mushi.
No comments:
Post a Comment