Mkuu wa Mawasiliano Chuo Kikuu cha Mzumbe Bi. Sylivia Lupembe
akimtambulisha Sia Nshiu mhitimu wa Programu ya Intrepreneuship "Trade
Promotion For Industrial Development" katika Chuo hicho ambaye yupo
katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADE
barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo akionyesha bidhaa zake za
kahawa na mvinyo huku Waziri wa viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage
akimsikiliza wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara RANTRADE Bw. Edwin Rutageruka.
Sia Nshiu mhitimu wa Programu ya Intrepreneuship "Trade
Promotion For Industrial Development" katika Chuo Kiku cha Mzumbe
akitoa maelezo ya bidhaa zake kwa Waziri wa viwanda na Biashara Mh.
Charles Mwijage wakati alipotembelea banda la chuo hicho katika
maonyesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kulia ni
Mkuu wa Mawasiliano Chuo Kikuu cha Mzumbe na wa pili kutoka ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara RANTRADE Bw. Edwin
Rutageruka.
Waziri wa viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijageakifurahia
jambo na Mkuu wa Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Bi. Sylivia
Lupembe wakati alipomaliza kutembelea katika banda hilo kushoto ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara RANTRADE Bw. Edwin
Rutageruka.
Bw Innocent Mgeta Afisa Udahili Mwandamizi akiwapa maelezo baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo.Bw Innocent Mgeta Afisa Udahili Mwandamizi akiwapa maelezo baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo.
Bi Sia Nshiu akitoa maelezo kwa Bi Masha Kimaku aliyetembelea katika banda hilo.
...............................................................................
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
WAHITIMU
wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro wameamua kutumia taaluma
ambayo wameipata chuoni hapo kufanya shughuli za ujasirimali kwa kubuni
bidhaa za kipekee.
Baadhi
za wahitimu hao ambao wamepikwa vema na Chuo Kikuu cha Mzumbe
wameonesha kwa vitendo kuwa elimu ambayo wanaipata chuoni hapo ni
mkombozi kwa Watanzania huku wakijivunia bidhaa ambazo wanazalisha kwa
ubora wa hali ya juu.
Mmoja
wa wahitimu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Sia Mshiu akiwa kwenye Banda la
Chuo hicho katika Maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea
viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam amesema kuwa kutokana na elimu
ambayo ameipata ameweza kuzalisha Wine na Kahawa.
“Elimu
ambayo nimeipata darasani imenifanya sasa niwe mjasiriamali na nimeweza
kubuni bidhaa zangu ambapo kwa sasa natengeneza Kahawa na Wine.
“Kahawa
ambayo naitengeneza ina ladha ya aina yake ambapo pia wakati wa
kuitengeneza nachanganya na viungo na hivyo kuwa na aina Fulani ya ladha
ambayo huwezi kuipata kokote zaidi ya kahawa ambayo
natengeneza,”amesema Mshiu.
Amefafanua
kutokana na kufanikiwa kutengeneza bidhaa hizo lengo lake ni
kuhakikisha anasajili Mamkala ya Chakula na Dawa(TFDA)na baadae Shirika
la Viwango Tanzania(TBS) ili kuifanya iwe rasmi na kuingiza sokoni.
Ametoa
ombi kwa Rais Dk.John Magufuli kuwa iwapo itawezekana anatamani kuona
kunaandaliwa mazingira mazuri ambayo yatajenga daraja la kuunganisha
wajasiriamali wadogo kama yeye na kisha kuwaunganisha na wawekezaji
wakubwa ili kuhakikisha siku moja nchi yetu inapiga hatua ya
kimaendeleo.
Chuo
kikuu cha Mzumbe kimeweka utaratibu wa kuhakikisha wanafunzi ambao
wamemaliza kwenye chuo hicho kuendelea kuwafuatilia na kuwaendeleza
katika shughuli ambazo wanazifanya.
No comments:
Post a Comment