HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 03, 2018

WASHINDI WA PROMOSHENI YA 'ONJA LADHA USHINDE' WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

KAMPUNI ya Unilever Tanzania Ltd, imekabidhi zawadi sh. 50,0000 kwa kila shindi kati ya saba huku wa nane akijinyakulia mbuzi, walioshiriki shindano la 'Promotion' ya Onja Ladha Ushinde.

Kampuni hiyo inajihusisha na kuzalisha bidhaa za Omo na Royco ambzo zimetengenezwa katika ubora wa viwango vinavyokublika sheria  katika masoko.

Akizungumza na katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Akofa At a, alisema promosheni hiyo iliandaliwa mahususi kwa mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan ambapo itaendelea hadi Julai 12 mwaka huu.

"Washindi hawa nane walipatikana baada ya kununua bidhaa zetu na kukwangua sitika iliyomo katika bidhaa zetu kisha kututumia namaba zake hata hivyo lengo letu nikutoa zawadi kwa washindi 100 kila wiki," alisema Ata.

Aliwataja washindi hao hao kuwa ni Rukia Yusufu, Emmy Ngasuga, Mussa Hassan, Mohamed Mlazi, Witness Mgoya, Onesmo Chengula na Ndula Rafael ambaye ameamu kuchukua mbuzi mwenye thaman ya sh. 50,000.

Aidha, alitoa rai kwa washindi na washiriki wengine kuendelea kununua bidhaa hizo mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza nfasi yao ya ushindi pia kufurahia ladha bora katika chakula kula huku wakiziweka katika usfi nguo zao kutokana na ubora wa zabuni ya Omo.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo iko kwaajili ya wananchi hivyo itaendelea kutoa bidhaa bora ili kukidhi matakwa ya wateja wao.

Meneja Masoko wa Unilever, Lumuli Minga, aliwaomba wananchi kutumia bidhaa zao na kushiriki kwenye promosheni zinazoandaliwa na kampuni hiyo kwani ni ya kweli na ndiyo maana washiriki walikabidhiwa zawadi zao mbele ya vyombo vya habari.

 "Unajua wapo ambao wanadhani tunafanya uzinguaji hapana hii ni kweli na kila atakayeshiki na kushinda atapewa zawadi yake hivyo wajitokeze kununua bidhaa zetu lakini pia washiri hizi promosheni," alisema Lumuli.

No comments:

Post a Comment

Pages