Kamanda Camillius Wambura (kushoto), akiwa na Abdurhaman Hamis wakishiriki Majimaji Selebuka Festival mjini Songea.
Wanariadha Mohamed Dulle na Geofrey Korosi wakichuana katika mbio za Kilomita 21 Majimaji Selebuka Marathon mjini Songea.
NA MWANDISHI WETU
TAMASHA la Majimaji
Selebuka 2018 limekata utepe jana mjini hapa kwa mbio za Marathon huku
ikishuhudiwa Nestory Hudu kutoka Singida akiwatoa nishai Wakenya.
Hudu aliibuka kidedea
katika mbio za Kilomita 42 kwa Wanaume akitumia saa 2:21:25 akifuatiwa na John
Leonard wa Arusha saa 2.22:09 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Simon Lelei
kutoka Kenya saa 2.22:54.
Kwa upande wa Wanawake
Kilomita 42 mshindi aliibuka Purity Biwott wa Kenya alishinda akitumia saa
2.43:59 akifuatiwa na Dorcus
Chesang pia wa Kenya aliyetumia saa 2.45:21 huku nafasi ya tatu ikienda
kwa Angel John wa Arusha
aliyetumia saa 2:53.44.
Kwa upande wa Kilomita
21 Wanaume Pascal Sarwat wa
Manyara alishinda akitumia saa 1.11:58 akifuatiwa na Samson Lyimo wa Songea saa 1.12:13 huku Mohamed Dulle wa
JWTZ Ruvuma akikamata nafasi ya tatu akitumia saa 1:12:34 wakati kwa Wanawake
Tabitha Kibeth wa Kenya alishinda akitumia saa 1.21: 34 kutoka Kenya akifuatiwa
na Violeth Adam wa Njombe akitumia 1.22:43 huku nafasi ya tatu ikikosa mshindi
Kwa upande wa Walemavu
Kilomita 21 mshindi aliibukaDavid Mabula akifuatiwa na John Stephano huku
nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Mathias Jollo wote kutoka Dar es Salaam.
Pia kulikuwa na Mbio
za Mita 800 kwa wanafunzi ambao walitia for a kwa mwitikio mkubwa na vipaji,
kwa wavulana Felix Ndunguru alishinda akitumia dakika 2.46:00 akifuatiwa na
Bashiru Ngonyani dakika 2:49.2 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Franco Justine
aliyetumia dakika 2:52.
Kwa wasichana Magreth
Thadei alitumia 2:58.53 akifuatiwa na Hadija Mohamed dakika 2:58.55 huku nafasi
ya tatu ikienda kwa Maisha Mwera dakika 2:59.03.
Mbali na washindi
kujizolea zawadi ya fedha taslimu na medali, pia walipata ofa ya kutembelea
Mbamba Bay Beach.
Majimaji Selebuka
Festival imeandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Songea-Mississippi
(SO-MI), kwa kushirikiana na Tanzania Mwandi chini ya udhamini wa Bakhresa
Group of Companies, Premier Bet, BIT Tech Ltd/Meridian Bet.
Akizungumzia tukio
hilo Mwenyekiti wa Riadha Mkoa wa Ruvuma, Christian Matembo, alielezea
kufurahishwa na muitikio wa washiriki mwaka huu ambao walifikia zaidi ya 200
walijitokeza huku watoto wakitia for a.
Baada yam bio, tamasha
linaendelea leo kwa maonyesho ya wajasiriamali, mashindano ya ngoma za asili.
No comments:
Post a Comment