NA
KENNETH NGELESI,MBEYA
LIGI ya soka na Netiboli Tulia Cup 2018 imezinduliwa
rasmi juzi katika Viwanja vya shule ya Msingi Ruanda Nzovwe jiji Mbeya huku
mdhamini wa michuano hiyo Naibu Spika Dk Tulia Ackson akizitaka timu za ligi kuu
zikiwemo Tanzania Prisons na Mbeya City FC kutumia michuano hiyo kusaka vipaji
vya wachezaji watakao weza kuwatumia katika michezo mbalimbali ikiwemo ligi
kuu.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa Michuano Dk.Tulia
alisema kuwa ligi hiyo itaanzia ngazi ya mitaa na baadaye kata 36 za jiji la
Mbeya ,ngazi ya sita bora nusu fainali na hatimaye fainali zinazotarajiwa kupigwa
Semptemba mwa huu.
Dk Tulia alisema ni fursa kwa timu za ligi kuu,daraja
la kwanza na pili lakini pia ni fursa kwa wachezaji kuonyesha uwezo wao wa
kucheza soka ili waweze kuonwa na timu kubwa .
‘Ni fursa kwa timu kusaka wachezaji lakini pia ni
fursa kwa kwa vijna kuonyesha uwezo wao kwani mpira kwa sasa ni ajira na si
soka tu lakini pia hata netibali itaenda sambamba kuanzi ngazi za mitaa na
hatiamiye kata’
Michuano hiyo ilizinduliwa kwa kuzikutanisha timu ya
Ilemi FC na Mbeya Youth mchezo uliomalizika Ilemi kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Dk Tulia alisema michujo utaanzai ngazi mitaa kwa ajili ya kuoputa bingwa wa
kata ambapo Tasisi yake “Tulia Trust” itatoa jezi pamoja na mpira kwa ajili ya
michezo ligi hiyo timu zote za
Katika hatua nyingine Dk. Tulia alibainisha zawadi kuwa
Bingwa katika michezo yote kila timu ataondoka na Bodaboda boda
moja,Kombe,Medali kila mchezaji,Seti ya Jezi,na mpira,washindi wa pili medali
kwa kila mchezaji,fedha taslimu sh.milioni 1.5,kombe,seti ya Jezi na Mpira.
Mshindi wa tatu ataondoka na fedha tasilimu milioni
moja,seti ya Jezi,mpira na medali kwa kila mchezaji,huku mshindi wan ne akiondoka
na shilingi lakini saba,700,000/ na watano shilingi laki tano na medali pia.
Pia Naibu Spika Dk Tulia alitangaza rasmi kugharamia
masomo ya ziada Binti Diana Lucas wa kidato cha nne kutoka shule ya Sekondari
Nzondahaki ya jiji Mbeya baada ya kufanya vizuri nafasi yan Ushambuliaji katika
mchezo wa soka wasichina kwenye Mashindano ya UMISETA 2018 yaliyiomalizika hivi karibuni jiji Mwanza.
Kwa upande wake Mdau wa mchezo wa soka jiji Mbeya
James Mwampondele alipongeza uamuzi uliofanywa na Naibu Spika huku akiahidi
kutoa seti moja ya Jezi kwa timu zitakazo shika nafasi ya kwanza hadi ya nne.
“Mimi naunga mkono kazi hii ya Naibu Spika hivyo
nikiwa kama mdau wa michezo nitatoa jezi seti moja kwa kila timu kuanzia ile ya
kwanza hadi itakayo shika nafsi ya nne”
No comments:
Post a Comment