*Ni wale wanaotuhumiwa kwa wizi wa dawa
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi watatu wa hospitali
ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa tuhuma za wizi dawa na vifaa tiba.
Pia
Waziri Mkuu ameahidi kuyafunga maduka yote ya dawa yanayodaiwa kununua
dawa kutoka kwa watumishi wa hospitali hiyo wasioukkuwa waaminifu na
kuziuza kwa wananchi.
Waziri
Mkuu amewasimamisha kazi watumishi leo (Jumatatu, Juni 30, 2018) wakati
alipotembelea hospitali ya wilaya hiyo akiwa katika ziara yake ya
kikazi mkoani Kigoma.
Amewataja
watumishi wanaotuhumiwa kuhusika na wizi huo kuwa ni Mfamasia wa wilaya
Bw. Michael Nindi, mtumishi wa maabara Bw. Tilas Mbombwe na Bibi.
Venansia Batega ambaye ni muuguzi.
“Watumishi
hawa nimewasimamisha kazi kuazia leo hii, ili wapisha uchunguzi wa
upetevu wa dawa na vifaa tiba zikiwemo darubini mbili. Hospitali hii
inamatatizo makubwa sana ya wizi,”.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amewataka watumishi wa umma kutenga siku tatu katika wiki na
kuwafuata wananchi waishio vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero zao na
kuzipatia ufumbuzi.
Pia
Waziri Mkuu amewataka watumishi hao waondoe urasimu wanaouweka kwa
lengo la kupokea rushwa na pia wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wa
aina yoyote.
“Sitarajii
kusikia jambo hilo kwa sababu halina nafasi. Vyombo vinavyosimamia
maadili ya utumishi vitimize wajibu wake ili kuwalinda wananchi
wasiingizwe katika utoaji rushwa,”.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JULAI 30, 2018.
No comments:
Post a Comment