Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la
Burigi na eneo la wananchi katika eneo la Nyungwe na Ofisa mwenye wadhifa wa
Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na Hifadhi
za Taifa Tanzania kusimamia Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa
Hifadhi za Taifa, Damian Saru ( wa kwanza kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU
HELELA-WMU).
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la
Burigi na eneo la wananchi katika eneo la Nyungwe na Meneja wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi
kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma
( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya Watumishi wa Mapori
ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na
kuwa Hifadhi za Taifa wakati
Naibu Waziri huyo alipotembelea jana
kwenye mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua
ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja
na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bihalamulo pamoja na
baadhji ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Bihalamulo.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa eneo la Ziwa Burigi katika eneo la Nkonje na Meneja wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi
kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma
( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga
akisaini kitabu cha wageni i katika eneo la Nyungwe wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde.
Baadhi ya mafuvu ya
wanayamapori katika Pori la A kiba la Burigi katika eneo la Nyungwe.
NA LUSUNGU HELELA-KAGERA
Bodi
ya Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na
kuruhusu matumizi ya bajeti ya mpito ya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni
zitumike kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi, uendelezaji utalii pamoja na
ujenzi wa miundombinu katika Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa
hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa.
Hatua
hiyo imekuja kufuatia tangazo la Serikali la kuyapandisha hadhi Mapori
ya Akiba ya Bihalamulo,Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi
za Taifa kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi
Kigwangalla wakati alipokuwa akihitimisha bajeti ya Wizara mwezi Mei
mwaka huu Bungeni mjini Dodoma.
Ofisa
Mwenye Wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi, Damian Saru amesema hayo jana mbele
ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga wakati
alipotembelea mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi ( BBK) ikiwa ni
ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya
kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori
hayo.
Alitaja fedha hizo
kuwa zimeshaanza kutumika katika kuimarisha ulinzi, kujenga miundo
mbinu ya utalii na Utawala, kuainisha mipaka , kusimamia mchakato wa
kupandisha hadhi mapori
Damian
Saru, Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na TANAPA,
aliwasilisha taarifa hiyo pamoja na kumweleleza Naibu Waziri huyo hatua
za utekelezaji zilizofikiwa katika mapori hayo.
Alimweleza kuwa askari 58 wameshafika kwenye mapori hayo matano kwa ajili ya kuongeza nguvu.
Mashine ya kutengeneza barabara ' Motor Grader moja imeletwa kwa sjiki ya kutengeneza barabara.
Pia,
Alimweleza Naibu Waziri huyo ikiwemo vitendea kazi ikiwemo ndege moja
magari manne, mahema silaha, GPS vimeletwa katika mapori hayo kwa ajili
ya kuimarisha utendaji kazi
Kufuatia
utekelezaji huo, Mkuu mwenye hadhi ya Mkuu wa Hifadhi alitaja mafanikio
yaliyopatikana katika kIpindi kifupi cha utekelezaji maagizo hayo kuwa
katika kipindi cha wiki mbili pamoja na ng'ombe 41 kukamatwa na
kufunguliwa mashtaka.
Pia , Alitaja idadi ya watuhumiwa 12
wa ujangili wamekatwa.
Aidha, Saru alitaja aina za vifaa vilivyokatwa kuwa ni mitumbwi mitatu, mkaa gunia mbili pamoja na baiskeli zopatazo 10.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri , Mhe.Hasunga ameridhishwa na hatua ya TANAPA
kwa ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA)
kwa nzuri waliyoifanya.
No comments:
Post a Comment