HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 24, 2018

MOTO WATEKETEZA NYUMBA-ZANZIBAR

Mabaki ya Nyumba ya Marehemu Maalim Rajab Mzee iliyopo Mtaa wa Rahaleo ambayo iliungua moto mapema asubuhi uliosababishwa na Hiter ya Umeme.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud wakifika katika eneo la tukio kuifariji na kuipa pole Familia ya Watoto Tisa ya Marehemu Maalim Rajab Mzee kufuatia Nyumba yao kuungua Moto.
Wa kwanza na wa Pili kutoka Kulia ni miongoni mwa Watoto  Tisa wa Familia ya Marehemu Maalim Jaba Mgeni wa Nyumba iliyoungoa Moto mapema asubuhi katika Mtaa wa  Rahaleo  wakimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  mkasa uliowapata wa kuunguliwa Nyumba yao.
Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kutoa pole na kuisisitiza Jamii kuwa na tahadhari ya matumizi salama ya huduma za Umeme ili kuepuka maafa.
Picha na – OMPR – ZNZ.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameinasihi Jamii Nchini kuwa na tahadhari kubwa wakati wa matumizi ya vifaa vya umeme ili kuwepuka madhara yanayoweza kuleta maafa makubwa hapo baadae.
Alisema Huduma ya umeme ni nzuri na muhimu katika matumizi ya mwanadamu kwenyea harakati zake na kimaisha za kila siku lakini inaweza kuwa janga iwapo mwanaadamu huyo ataamua kutumia huduma hivyo ovyo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo muda mfupi tu alipopata taarifa ya kutokea kwa Janga la Moto katika Nyumba ya Familia ya  Marehemu Maalim Rajab Mgeni iliyopo Rahaleo mbele ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Muembe Shauri.
Hata hivyo hakuna mtu aliyepata matatizo kutokana na mripuko wa moto huo uliosababishwa na kuungua kwa Hita iliyokuwemo kwenye Nyumba hiyo ambayo wakati inawaka alikuwemo Kijana Mmoja wa familia ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda maisha na mali za Rais imeazimia kujenga Vituo vya Huduma za Zimamoto kila Wilaya kwa lengo la kuwa tayari wakati yanapojitokeza matukio ya majanga.
“ Umeme tunaupenda  sana katika matumizi yetu ya kawaida ya kila siku lakini pia unahatari iwapo hatutakuwa makini katika matumizi yake ya ovyo”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikipongeza Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar kwa umakini wake uliopelekea kuuzima moto huo kwa dakika chake na kuepusha maafa ya kuendelea kuathiri nyumba zilizo jirani na eneo hilo.
Balozi Seif pia akalipongeza Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC – REDIO} kwa kuwapasha Wasikilizaji Wananchi katika mfumo wake wa matangazo wa moja kwa moja wa haraka { Breakingnews} ambao ulisaidia baadhi ya Wananchi wa karibu na maeneo hayo kufika mara moja kusaidia kuiokoa Nyumba hiyo.
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  alisema licha ya uharaka na utayari wa Wananchi na vyombo vya Dola katika kuokoa maafa lakini bado lipo changamoto kubwa la baadhi ya Wananchi kujenga makaazi yao bila ya kuzingatia mipango miji.
Balozi Seif  alieleza kwamba ujenzi wa nyumba  katika baadhi ya maeneo bila ya kufuata  utaratibu wa ujenzi hupelekea Kikosi cha Zima moto na Uokozi kupata usumbufu wakati wa majanga kutokana na Magari yao kusindwa kupenya katika baada ya Mitaa.
Nyumba hivyo ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni iliyorithiwa na Watoto Tisa hapo Rahaleo iliyoungua majira ya saa Moja na Robo asubuhi imeteketea kwa moto na hakuna kitu kilichopatikana ndani sambamba na kutofahamika hasara yake hadi hivi sasa.
 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
24/08/2018.

No comments:

Post a Comment

Pages