Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili katika
Gereza la Wilaya Singida leo Agosti 23, 2018 tayari kwa ziara yake ya kikazi ya
siku moja yenye lengo la kukagua shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi
hilo Mkoani Singida.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (katikati) akiongea na Maafisa na askari
wa Magereza Mkoani Singida kabla ya kutembelea Magereza mbalimbali ya Mkoa humo (kulia)
ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa Singida, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Omary
Msepwa.
Askari wa vyeo mbalimbali wa Gereza Singida
wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza.
Mkuu wa Gereza Ushora, Mrakibu wa Magereza,
Kulwa Kabota (katikati) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike (wa kwanza kushoto) mashine ya kukamulia arizeti leo Agosti 23, 2018
alipotembelea Gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike akikagua tanuru la tofali za kuchoma katika eneo la Gereza la Kilimo na
Mifugo Ushora, lililopo Mkoani Singida. Tofali hizo za kuchoma hutumika kujenga
nyumba za watumishi katika Magereza mbalimbali Mkoani Singida pamoja na ujenzi
wa mabweni ya wafungwa.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike (mwenye miwani) akikagua ujenzi wa nyumba ya makazi ya askari wa Gereza
la Kilimo na Mifugo Ushora, Mkoani Singida alipofanya ziara ya kikazi leo
Agosti 23, 2018.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (kushoto) akikagua ghala la kuhifadhia arizeti
ambayo imevunwa na kupepetwa tayari kwa ukamuaji wa mafuta ya arizeti ambayo
hutumika kwa chakula cha wafungwa Gereza Ushora lililopo Singida.
. Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na askari wa kike wa Magereza Mkoani Singida leo katika ziara yake ya
siku moja Mkoani humo. Jenerali Kasike katika ziara hiyo ya siku moja ametembelea
Gereza la Wilaya Singida na Gereza la Kilimo na UfugajiUshora kabla ya kuelekea jijini Dodoma kuendelea na majukumu mengine ya kitaifaPicha
zote na Jeshi la Magereza
Na Lucas Mboje,
Singida
MKUU
wa Jeshi la Magereza nchini – CGP Phaustine Kasike ameonya
vikali tabia ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wanaojihusisha na
matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo ni kinyume na kanuni
za uendeshaji wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali Kasike amesema hayo leo Alhamisi
katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza
changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo Magereza Mkoani Singida.
Amesema kuwa limezuka wimbi la askari wa Jeshi
hilo kutumia vibaya mitandao ya kijamii kinyume na maadili ya Jeshi hilo kwa baadhi ya askari kuitumia vibaya kuchangia na kutoa maoni katika mitandao ya kijamii
mambo yasiyofaa.
Jenerali
Kasike amewataka askari wote nchini
kuepuka kulichafua jeshi hilo mbele ya jamii badala yake wanatakiwa kuwa kielelezo
kwa Taifa.
“Niwasihi
sana jiepusheni na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii bali itumieni
kupashana habari za msingi na zenye manufaa kwenu kwani nafahamu mitandao ya
kijamii inarahisisha kupashana habari kwa uharaka zaidi.” Alisisitiza Jenerali
Kasike.
Aidha,
Kamishna Jenerali Kasike ameongeza kuwa
Jeshi hilo halitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu askari yeyote
atakayebainika kutenda makosa hayo ya kimaadili kwani yanalifedhehesha Jeshi la
Magereza mbele ya jamii.
Kuhusu upungufu wa nyumba za kuishi
kwa watumishi wa Jeshi hilo, Jenerali Kasike amewataka wakuu wote wa magereza
nchini kuwa wabunifu hususani katika kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao
ikiwemo fursa ya kufyatua tofali za kuchoma ili kupunguza tatizo hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Kilimo
na Mifugo Ushora, Mrakibu wa Magereza Kulwa Kabota ameushukru Uongozi wa Jeshi
la Magereza kwa kuwawezesha kiasi cha Shilingi Milioni 9 ambazo zitasaidia
kukamilisha ujenzi na upauaji wa nyumba ya askari katika gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini,
Phaustine Kasike yupo katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Singida ambapo
amekagua Gereza la Wilaya Singida na Gereza la Kilimo na Ufugaji Ushora kabla
ya kuelekea jijini Dodoma kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.
CAPTIONS
PIX 1. Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili katika
Gereza la Wilaya Singida leo Agosti 23, 2018 tayari kwa ziara yake ya kikazi ya
siku moja yenye lengo la kukagua shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi
hilo Mkoani Singida.
PIX 2. Kamishna
Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiongea na Maafisa na askari
wa Magereza Mkoani Singida kabla ya kutembelea Magereza mbalimbali ya Mkoa humo(kulia)
ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa Singida, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Omary
Msepwa.
PIX 3. Askari wa vyeo mbalimbali wa Gereza Singida
wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza.
PIX 4. Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike akikagua tanuru la tofali za kuchoma katika eneo la Gereza la Kilimo na
Mifugo Ushora, lililopo Mkoani Singida. Tofali hizo za kuchoma hutumika kujenga
nyumba za watumishi katika Magereza mbalimbali Mkoani Singida pamoja na ujenzi
wa mabweni ya wafungwa.
PIX 5. Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike(mwenye miwani) akikagua ujenzi wa nyumba ya makazi ya askari wa Gereza
la Kilimo na Mifugo Ushora, Mkoani Singida alipofanya ziara ya kikazi leo
Agosti 23, 2018.
PIX 6. Kamishna
Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(kushoto) akikagua ghala la kuhifadhia arizeti
ambayo imevunwa na kupepetwa tayari kwa ukamuaji wa mafuta ya arizeti ambayo
hutumika kwa chakula cha wafungwa Gereza Ushora lililopo Singida.
PIX 7. Mkuu wa Gereza Ushora, Mrakibu wa Magereza,
Kulwa Kabota(katikati) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike( wa kwanza kushoto) mashine ya kukamulia arizeti leo Agosti 23, 2018
alipotembelea Gereza hilo.
PIX 8. Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine
Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na askari wa kike wa Magereza
Mkoani Singida leo katika ziara yake ya siku moja Mkoani humo. Jenerali Kasike katika
ziara hiyo ya siku moja ametembelea Gereza la Wilaya Singida na Gereza la Kilimo
na UfugajiUshora kabla ya kuelekea jijini Dodoma kuendelea na majukumu mengine
ya kitaifaPicha zote na Jeshi
la Magereza).
No comments:
Post a Comment