Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano),
Mhandisi Atashasta Nditiye akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw Richard Mayongela kabla ya kuanza kwa
kikao cha mrejesho wa utekelezaji mbalimbali. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Watu Mashuhuri wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA).
3. 7:
4. Selected:
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard
Mayongela.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano),
Mhandisi Atashasta Nditiye (Kushoto) akizungumza jambo mbele ya waandishi wa
habari katika kikao cha mrejesho wa
utekelezaji wa maelekezo aliyotoa katika ziara zake za nyuma. Kikao
hicho kilifanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA).
Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta bya Uchukuzi na
Mawasiliano), Mhandisi Atashasta Nditiye, (kushoto), akizungumza na waandishi w
ahabari kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam leo Agosti 30, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa amlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Bw. Richard Mayongela.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta
Nditiye, ameagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kushirikiana
na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, wakakague viwanja 537 vilivyotengwa maeneo ya
Msongola, kwa ajili ya waliokuwa wakazi wa eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam
Jumanne wiki ijayo ili kujiridhisha kama viwanja hivyo vipo na vinafaa.
Mhandisi Nditiye ametoa agizo hilo leo Agostri 30, 2018, wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwe nye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo alieleza wasiwasi wake kuwa kampuni
iliyopewa kandarasi ya kuwatafutia viwanja wananchi hao haijatekeleza wajibu
wake ipasavyo licha ya kuwa tayari imelipwa kiasi cha shilingi bilioni 3.7.
“Nakuagiza Mkurugenzi wa TAA, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa
Wilaya Jumanne ijayo muende mkakague eno hilo la viwanja 537 muone kama vipo
kwa sababu kumekuwa na shida sana na hawa wenzetu wa Tanzania Remix Centre
nyinyi wenyewe mnajua, kuna shida ya miundombinu, sasa lazime mjue eneo hilo
linafikika, na viwanja hivyo vinajengeka.” Alisema
Alisema Wananchi wako tayari kushirikiana na serikali katika
kuhakikisha upanuzi wa uwanja unakwenda vizuri.
Kampuni ya Tanzania Remix Centre ilipendekezwa na Manispaa
ya Ilala na kupewa kandarasi ya kutafuta viwanja kwa ajili ya makazi
mapya ya wananchi waliokuwa wakiishi eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo kulikuwepo na mivutano kati ya Mamlaka na Wananchi
ambapo baadhi yao walipeleka shauri hilo mahakamani na hiovyo kufanya zoezi
hilo la kuwahamisha wananchi hao kwenye eneo hilo jipya kusuasua.
Hata hivyo akitoa taarifa kwa Mhe. Naibu Waziri Nditiye,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.Richard
Mayongela alisema, Novemba mwaka jana, TAA ilikutana na wadau wakiwemo
wananchi, Manispaa ya Ilala, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kampuni iliyoingia ubia
na Manispaa ya Ilala katika kutafuta viwanja kwa ajili ya wananchi hao.
“Mradi huu ulihusisha upatikanaji wa viwanja 1,600 kwa mujibu wa
mkataba wa awali ambapo fidia yake ilipaswa kufanywa kwa awamu mbili ya watu
800, hata hivyo kwa mujibu wa sheria kipinde kile ilitaka mwananchi apewe eneo
lakini alipwe fidia pia.” Alisema na kufafanua kuwa.
“Sasa wananchi wa Kipawa na Kigilagila walilipwa fidia kwa mujibu
wa sheria na kwao hakukuwa na tatizo, kwa maana walipewa fedha taslimu na
viwanja maeneo ya Pugu Mwakanga.” Alisema Bw. Mayongela
Akieleza zaidi Bw. Mayongela alsiema Baada ya kufanya tathmini,
ilibainika kuwa wananchi wa Kipunguni A na Kipunguni Mashariki ambapo kulikuwa
na viwanja 1,186 baada ya kufanya tathmini viwanja vilivyohitajika siyo 1,600,
bali ni 1,186, kwa ajili ya fidia ya wananchi wa maeneo hayo mawili na katika
viwanja hivyo viwanja 537 serikali ilishatoa kiasi cha shilingi bilioni 3.7 ili
kutekeleza zoezi hilo.
Sisi kwa kushirikiana na mbia wa Mnaispaa ya Ilala yaani Tanzania
Remix Centre, tukaandaa vile viwanja na viwanja vile vimeshapatikana na
kuanzia hivi sasa, viwanja hivyo vitagawiwa kwa wananchi.
Aidha katika hatua nyingine, Mhe. Nditiye amesema wakati umefika
sasa kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, kuanzisha kitengo cha Estate ili kihakikisha
viwanja vyake vyote nchini vinakuwa na hati miliki.
“Naguagiza uunde kitengo cha Estate kisichozidi watu 10 ili
kihakikishe kila kiwanja kinachomilikiwa na TAA kinakuwa na hati miliki na hii
itaepusha migogoro na wananchi.” Alisema.
No comments:
Post a Comment