NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), inashiriki
katika maonyesho ya Nanenae yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi
Mkoani Simiyu.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo, alisema kuwa kauli mbiu ya maonyesho ya Nanenane mwaka 2018 ni 'Wekeza
katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda.'
Katika
maonyesho ya Nanenane Mkoani Simiyu, NSSF inatoa huduma mbalimbali zikiwemo
elimu kwa umma juu ya Wakulima Scheme.
Lengo la
Wakulima Scheme ni kutoa mafao yote yanayotolewa na NSSF kwa wanachama walio
katika sekta ya kilimo.
Kwa
kujiunga na NSSF wakulima na familia zao wanaweza pata matibabu ya bure, pia
NSSF inawawezesha kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kununulia pembejeo,
kusomesha watoto wao na kufanya shughuli zingine za kimaendelo.
Huduma
zingine zinazotolewa katika banda la NSSF ni pamoja na elimu ya mafao na
umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa watu walio katika sekta binafsi na sekta isiyo
rasmi, kuadikisha wanachama wapya, kutoa taarifa za michango ya wanachama na
maelezo juu ya miradi ya nyumba zinazouzwa na Shirika, viwanja na majengo ya
kupangisha.
NSSF
inawakaribisha wakazi wote wa Simiyu na maeneo ya jirani wafike katika banda la
NSSF lililopo pembeni ya mabanda ya Benki ya NMB na NBC ili waweze kupata huduma
za NSSF kwa ajili ya kuboresha maisha ya sasa na baadae.
Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Omary Mgumba akisikiliza
maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa NSSF kwenye maonyesho ya Nanenae
Simiyu.
Afisa wa NSSF Hamisi Duma akitoa maelezo kwa wakina mama
waliotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.
Afisa wa NSSF Hamisi Duma akitoa maelezo kwa wakina mama
waliotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.
Afisa wa NSSF Khali Abubakar akitoa maelezo kwa mkazi wa Bariadi
aliyetembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.
Afisa wa NSSF Mario Zemba akitoa maelezo kwa mwanachama
aliyetembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.
Afisa wa NSSF Mselem Mwanamsoga akitoa maelezo kwa mwanachama
aliyetembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.


No comments:
Post a Comment