HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 09, 2025

Usalama wa uwekezaji UTT AMIS, namna inavyopunguza hatari kwa wawekezaji

KATIKA mazingira ambapo ukosefu wa taarifa sahihi umekuwa chanzo kikuu cha hofu kwa wawekezaji, UTT Asset Management and Investor Services (UTT AMIS) imeendelea kuwa mfano wa taasisi yenye uwazi, nidhamu ya kifedha na ulinzi madhubuti wa mali za umma. 


Ilianzishwa chini ya Wizara ya Fedha mwaka 2003 na kuanza rasmi mwaka 2005, UTT AMIS imejijengea rekodi ya zaidi ya miaka 20 bila tukio lolote la kupotea kwa fedha za wawekezaji jambo ambalo halitokei kwa bahati, bali matokeo ya mifumo thabiti ya usimamizi na kupunguza hatari za uwekezaji.

Usimamizi wa kisheria, kiserikali

UTT AMIS ni taasisi ya Serikali, ikifanyakazi chini ya usimamizi wa karibu wa Capital Markets and Securities Authority (CMSA)–mamlaka inayoidhinisha, kusimamia na kuhakikisha kila mfuko unaendeshwa kwa mujibu wa sheria za soko la mitaji.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inahakikisha nidhamu ya kifedha, usalama wa shughuli na utunzaji sahihi wa mali.

Uwepo wa taasisi hizi mbili hutoa uangalizi wa mara mbili, yaani uwekezaji una angalia na macho ya kampuni mbili, jambo linalowapa wawekezaji uhakika uliodhibitiwa na Serikali.


Mali za wawekezaji zimetenganishwa 


Fedha za wawekezaji hazina uhusiano wa kifedha na uendeshaji wa UTT AMIS. 

Kisheria, mali zote huwekwa kwenye “trust structure” kwa niaba ya wawekezaji na haziwezi kutumika kwa madhumuni mengine nje ya uwekezaji uliokusudiwa. 

Hii inalinda uwekezaji hata kama taasisi ingekumbana na changamoto.


3. Ushiriki wa benki huru kama mwangalizi

Mali za wawekezaji zinatunzwa na benki kubwa nchini CRDB

Benki hii ndiyo inayo hifadhi rasmi mali za wawekezaji. 

Hivyo kuna ngazi ya ziada ya ulinzi, UTT AMIS haisogei moja kwa moja kwa mali bali huzisimamia kiuwekezaji tu.



Uwekezaji unaozingatia usalama na utulivu


Mfuko huwekeza kwenye bidhaa salama za kifedha kama: Hati fungani za Serikali za muda mrefu (Government Bonds) na za muda mfupi (Treasury Bills), Fixed deposits za benki kubwa.

Pia hatifunguni za Kampuni kubwa -corporate bonds.

Mchanganyiko huu hupunguza hatari ya mtikisiko wa soko kwa kuwa asilimia kubwa ya mali ziko kwenye vyombo vya Serikali ambavyo ni salama na vinatoa mapato ya uhakika.


Ukaguzi huru wa kila mwaka

Kila mfuko hupitia ukaguzi huru unaofanywa na wakaguzi walioidhinishwa na Serikali. 

Ripoti hizi huwa hadharani, jambo linaloongeza uwazi na uaminifu kwa wawekezaji.


Risk Mitigation


Hii ni namna UTT AMIS inavyolinda uwekezaji

Ili kuhakikisha uwekezaji wa Mtanzania unakuwa salama, UTT AMIS hutumia mbinu kadhaa za kisasa za kupunguza hatari:

Uwekezaji ni katika makapu mbalimbali ili kukwepa mayayi yote kuvunjika pale kapu moja linapo anguka.

Uwekezaji hausongwi mahali pamoja. Fedha zinagawanywa kwenye, Hati fungani, Soko la hisa na Fedha taslimu.

Ugawaji huu hupunguza hatari ya kupoteza thamani ikiwa chombo kimoja cha uwekezaji kitapata changamoto.


Utaalamu


Wataalamu wa uwekezaji walioidhinishwa na CMSA huongoza maamuzi yote. Wanachambua masoko, tathmini hatari na kufanya maamuzi ya kitaalamu ili kulinda mtaji na kukuza thamani kwa muda mrefu.

Kufuata Miongozo ya Hatari (Risk Limits & Compliance).

Kila mfuko una vigezo au mipaka ya kiasi cha kuwekeza mfano, Kiasi cha juu kinachoweza kuwekezwa kwenye hisa.

Kiwango kinachotakiwa kwenda kwenye hati fungani na muda wa hati fungani zinazoruhusiwa.

Miongozo hii huweka uwiano wa hatari unaokubalika.



Ustahimivu


UTT AMIS hufanya majaribio ya kuangalia kama mfuko unaweza kustahimili: Mabadiliko makubwa ya riba, Kuporomoka kwa soko na Msukosuko wa uchumi.

Hii hujenga uwezo wa kupambana na misukosuko ya kifedha.


5. Liquidity Management


Mfuko husimamiwa ili kuhakikisha: Kuna fedha za kutosha kwa ajili ya malipo ya wateja,

hakuna shinikizo la kuuza mali kwa hasara na 

hii ndiyo sababu wawekezaji huweza kupata pesa zao bila kikwazo.


Hitimisho

Kwa zaidi ya miaka 20, UTT AMIS imejijengea nafasi ya kipekee kama taasisi salama na ya kuaminika kwa watanzania wanaotafuta uwekezaji wa muda mrefu. 

Kwa muundo wake wa kisheria, usimamizi wa Serikali, custodian benki, ukaguzi huru na mbinu za kisasa za kupunguza hatari, UTT AMIS imeendelea kuwa kimbilio la wawekezaji wadogo, wa kati na wakubwa.







No comments:

Post a Comment

Pages