Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga, akizungumza
na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili
na utalii wakati akifungua kikao cha
kutathimini hatua zilizofikiwa katika ukamilishaji wa taratibu za uanzishwaji
rasmi wa Jeshi Usu kilichofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt.
Aloyce Nzuki.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga ( wa pili kulia) akifungua kikao
cha Wenyeviti wa Bodi pamoja na Wakuu wa
Taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Maliasili na utalii kwa ajili ya kutathimini hatua zilizofikiwa katika
ukamilishaji wa taratibu za uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu. Wa kwanza kulia ni
Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki. Wa kwanza kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Prof. Abiud Kaswamila
pamoja na Kamishna wa Operesheni na
Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi
ya TANAPA.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga ( katikati) akizungumza na
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania, Allan Kijazi wakati alipokuwa akiwasili kwa ajili ya kikao
na Wenyeviti wa Bodi pamoja na Wakuu wa
Taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Maliasili na utalii kilichofanyika jijini Arusha.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani ( wa
kwanza)ambaye pia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa
akizungumzia hatua za kuchukua katika uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu,
Mjumbe wa Sekretarieti wa hatua za
uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu ambaye ni
Mwanasheria Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meinrad Rweyemamu akitoa ufafanuzi wa
kisheria kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga jana
kwenye kikao kwa Wenyeviti na wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo
kilichofanyika jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii( wa
kwanza kushoto) akizungumza na Wenyeviti wa Bodi zilizo chini ya Wizara ya
Maliasili na utalii kwenye kikao cha
kutahimini hatua zilizofikiwa katika ukamilishaji wa taratibu za
uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Japhet Hasunga. (PICHA ZOTE NA
LUSUNGU HELELA)
No comments:
Post a Comment