NA
SALUM MKANDEMBA
MUIGIZAJI
mahiri wa vichekesho wa Kundi la Futuhi, linalorusha michezo yao kupitia
StarsTv, Dickson Pamba maarufu kwa jina la Karume Kenge (pichani), amefariki dunia leo
alfajiri baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa
mujibu wa muigizaji mwenzake wa Kundi la Futuhi, Sharobaro wa Kihaya, Karume
Kenge amefariki dunia saa 10 alfajiri ya kuamkia Jumamosi Oktoba 27, wakati
akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Jijini Mwanza.
“Ni
kweli Karume Kenge amefariki dunia alfajiri ya leo majira ya saa 10 katika
Hospitali ya Rufaa ya Bugando, tayari mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha
maiti hospitalini hapo,” alisema Sharobaro.
Aliongeza
kuwa, mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Nyegezi na kwamba hawajajua
atazikwa lini kwa sasa, ingawa familia inafikiria kusafirisha mwili wa marehemu
kwenda kuzikia kwao Ukerewe mkoani humo.
Karume
Kenge ni msanii wa pili wa Kundi la Futuhi kufariki dunia, baada ya Omary Dude ‘Mzee
Dude,’ kufariki dunia jioni ya Januari 27 mwaka 2014, katika hospitali
hiyo hiyo ya Bugando alikokimbizwa hapo siku moja kabla.
Mzee
Dude alifariki dunia kutokana na maradhi ya figo na kutokana na kifo chake na
hiki cha sasa cha Karume Kenge, inalifanya Kundi la Futuhi kubakiwa na wasanii
Sharobao wa Kihaya, Brother K ‘Wa Kukurupuka’, Mama Njelekela, Gongalai, Mjaluo
na Njelekela ‘Emoro’.
No comments:
Post a Comment