Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Bi. Doris Uhagile (katikati) leo akiwa eneo la ukaguzi wa tiketi za abiria ambapo alitoa maelezo ya namna mashirika ya ndege yavyohudumia abiria kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwelwe. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya TAA, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema. (Na Mpiga Picha Wetu).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwelwe (kulia) leo akimsikiliza Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Bi. Doris Uhagile (katikati), akimpa maelezo mbalimbali wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye kiwanja hicho. Mwenye tai nyekundu ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyangu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwelwe (kulia) leo akimsikiliza Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Bi. Doris Uhagile (katikati), akimpa maelezo mbalimbali wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye kiwanja hicho. Mwenye tai nyekundu ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyangu.
1.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhe. Isack Kamwelwe akipita eneo la ukaguzi wa abiria na mizigo la Kiwanja cha
Ndege cha Bukoba, leo alipofanyua ziara ya kikazi. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Ushari (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prof.
Ninatubu Lema.
Na
Mwandishi Wetu, Bukoba
SERIKALI
inafikiria kufanya upanuzi na urefushaji wa barabara ya kutua na kuruka kwa
ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Bukoba licha ya changamoto zilizopo, ili
kiruhusu kutua kwa ndege kubwa zaidi.
Hayo
yamesemwa leo (jana) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Isack Kamwelwe katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu ya taasisi
zilizopo chini ya Wizara yake, ambapo kiwanja hicho kipo chini ya Mamlala ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Mhe.
Kamwelwe amesema bado Kiwanja hicho kinakabiliwa na changamoto endapo
kitaongezwa lazima baadhi ya nyumba za Ibada, hospitali na nyumba za kuishi
watu zitalazimika kuondolewa ili kupisha upanuzi huo.
“Ukiangalia
upande mmoja unamakazi ya watu na upande mwingine ni Ziwa Viktoria na mwingine
kuna Mlima, hivyo bado tunafanyia kazi hizi changamoto na endapo zitatatuliwa
basi miundombinu hii itaboreshwa zaidi kwa kuwa tayari lipo jengo zuri na lenye
mfumo mzuri wa maji taka na mifumo mingine mbalimbali,” amesema Mhe. Kamwelwe.
Hata
hivyo, amesema Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) litaongeza safari zake mara
mbili kwa siku wenye Kiwanja cha ndege cha Bukoba, kutokana na kuwa na abiria
wengi kwa sasa.
Mhe.
Kamwelwe amesema kwa sasa ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 inakuja mara moja
kwa siku kwa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.
“Kwa
sasa abiria wameongezeka zaidi nimeelezwa kuwa kwa mwaka ilikuwa kiwanja
kinaweza kuhudumia abiria 28,000 pekee, lakini sasa ni zaidi ya 45,000 kwa
mwaka, hivyo inaonesha ni kiasi gani wanavyoongezeka na ndio maana ninasema
kutakuwa na uwezekano wa kuongeza safari za ATCL na iwe mara mbili kwa siku
balada ya sasa mara moja,” amesema Mhe. Kamwelwe.
Amesema
serikali tayari imenunua ndege mbili aina ya Airbus 220 zenye uwezo wa kubeba
abiria 132 zitakazowasili nchini Desemba 18 na 23, 2018 tayari kwa safari za
maeneo mbalimbali.
Ndege
hizi zinaweza kutua kwenye viwanja vya ndege vya daraja la 4C, ambapo kwa sasa
ni Songwe na Mwanza, na baada ya ukarabati kukamilika kwenye kiwanja cha Mtwara
na kuboreshwa kwa Kigoma, pia itaweza kutua; hali kadhalika pia itatua kwenye
viwanja vya Kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA) na Kilimanjaro (KIA), ambavyo
ni daraja la 4E.
Kiwanja
cha Ndege cha Bukoba kinajengo la kisasa la abiria, ambalo lilizinduliwa
Desemba 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, ambapo mbali na
ATCL ndege nyingine zenye ratiba maalum zinazotua ni pamoja na Precision, wakati
nyingine zinakuwa zimekodiwa bila kuwa na ratiba maalum kama Auric.
No comments:
Post a Comment