Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bahati Gauzye, akizungumza katika hafla ya Kutunuku hati za Utambuzi wa Elimu kwa
Wafadhili na Wachangiaji katika Mfuko wa Elimu.
Mwenyekiti
wa Bodi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Prof. Maurice Mbago,
akizungumza katika hafla ya Kutunuku hati za Utambuzi wa Elimu kwa
Wafadhili na Wachangiaji katika Mfuko wa Elimu.
Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya Kutunuku hati za Utambuzi wa Elimu kwa Wafadhili na Wachangiaji katika Mfuko wa Elimu.
Wadau mbalimbali waliochangia Elimu wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akimtunuku hati ya Utambuzi katika Elimu, Jacqueline Mengi, ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dk. Ntuyabaliwe, wakati wa hafla ya kutunuku hati hizo kwa wafadhili na wachangiaji 18 wa elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) jijini Dar es Salaam.
Wadau.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akimtunuku hati ya Utambuzi katika Elimu, Ofisa Mahusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Kilo Mgaya, wakati wa hafla ya kutunuku hati hizo kwa wafadhili na wachangiaji 18 wa elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Benki ya CRDB akiwa na cheti alichokabidhwa.
Wadau mbalimbali.
Wadau wa elimu wakiwa katika hafla hiyo.
Bendi ikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafadhili na wachangiaji wa Elimu.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Naibu
Waziri wa Elimu, William Ole Nasha, akibadilishana mawazo na Mwenyekiti
wa Bodi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Prof. Maurice Mbago.
Naibu
Waziri wa Elimu, William Ole Nasha (kulia), akiagana na Mwenyekiti
wa Bodi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Prof. Maurice Mbago.
Naibu
Waziri wa Elimu, William Ole Nasha, akiagana na Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bahati Gauzye.
NA
JANETH JOVIN
SERIKALI
imesema katika kipindi cha miaka mitatu
imepokea Sh. Bilioni 11 kutoka kwa wafadhili na wachangiaji 18 wa elimu waliopo
nchini na nje ya nchi.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha, alitoa kauli hiyo
jijini Dar es Salaam jana wakati wa
hafla ya kutunuku hati ya utambuzi katika elimu kwa wafadhili na wachangiaji 18
wa elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Ole
Nasha alisema kiasi hicho cha fedha kimetumika na kinaendelea kutumika
kutengeneza madawati, ujenzi wa maktaba, mabweni, madarasa, kutengeneza miundombinu ya maji pamoja na
usambazaji wa vitabu katika shule na vyuo vikuu mbalimbali vya serikali nchini.
"Pia
ripoti zote za ufatiliaji wa fedha hizi zipo na zinazotolewa hivyo natoa rai
kwa TEA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hakikisheni kuwa ziwafikie haraka,
ili waliotoa fedha waone ni kwa jinsi gani zimetumika katika malengo
yaliyokusudiwa," alisema.
Aidha,
Ole Nasha alisema serikali kwa mwaka huu inatarajia kukusanya Sh. Bilioni 400
kutoka kwa wadaiwa sugu wa mikopo nchini.
Alisema
pamoja na malengo hayo, katika kipindi cha miaka mitatu marejesho ya mikopo
hiyo yameongezeka kutoka Sh. Bilioni 20 mwaka 2016/17 hadi kufikia Bilioni 184
2017/18.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Prof. Maurice Mbago, alisema hati hizo zinazotolewa
na wao kwa kushirikiana naTRA zina lengo la kutambua mchango wa wafadhili wa
elimu katika kuchangia fedha za kujenga majengo na ununuzi wa vifaa mbalimbali
kwa ajili ya masuala ya elimu.
Alisema
pamoja na utoaji wa hati hizo bado wanakabiliwa na changamoto ya uwepo wa
mwamko mdogo na uelewa hafifu kwa baadhi ya kampuni juu ya manufaa ya kuchangia miradi ya elimu
nchini.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Dk. Ntuyabaliwe ambayo ni miongozi wa wadau wa elimu waliopata
hati hizo, Jacqueline Mengi, aliishukuru Serikali kwa kutambua mchango wake
katika sekta ya elimu.
Alisema
taasisi yake itaendelea na programu za kujenga maktaba, usambazaji wa vitabu
vya hadithi pamoja na uendeshaji wa shindano la kuandika hadhiti lijulikanayo
'Andika Challenge ' katika shule mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment