·
SuperSport yapata idhini kuonyesha mechi zote za michuano hiyo
·
Wababe wa Soka Afrika Mashariki kutunishiana misuli
·
Mshindi kupata fursa ya kucheza na Everton FC
Dar es Salaam, Tanzania - Jumanne, 15 Januari 2018 ---
Wapenzi wa kandanda Afrika Mashariki, wanauanza mwaka huu kwa burudani
ya aina yake kwa kushuhudia mubashara michuona maarufu ya Kombe
la SportPesa itakayoonyeshwa ndani ya DStv kupitia SuperSport ambayo
imepata idhini ya kuonyesha michuano hiyo kama mshirika rasmi.
Michuano
hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam itahusisha vigogo 8 wa soka
kutoka Tanzania na Kenya na itatimua vumbi kuanzia Januari 22 hadi 27.
Michuano hiyo itakuwa na mvuto wa aina yake
hasa ukizingatia ukubwa na umaarufu wa timu zinazoshiriki zikiwemo
watani wa jadi Simba na yanga, Mbao FC pamoja na Singida United kutoka
Tanzania na vigogo wa soka Gor Mahia, AFC Leopard, Bandari FC and
Kariobangi Sharks kutoka Kenya
Michuano
hiyo itakuwa na mvuto wa aina yake kwani mbali na ukubwa, umaarufu na
utani wa timu shiriki, pia kila timu itataka kutwaa kombe hili na
hatimaye kupata fursa ya kucheza na moja ya timu
maarufu ya soka nchini Uingereza – Everton FC
No comments:
Post a Comment