Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga (katikati), akimtambulisha kocha mpya wa timu hiyo, Mserbia Dragan Popadic (kushoto), akiwa na msaidizi wake, Dusan Momcilovic. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI WETU
UONGOZI
wa Singida United, umevunja benki kwa kuwasajili makocha wawili kutoka Serbia
kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo, ambayo msimu huu imekuwa haina makali sana.
Timu
hiyo imemleta Dragan Popadic ambaye atakuwa Kocha Mkuu na kuamua kuja na Msaidizi
wake, Dusan Momcilovic.
Singida
United imemleta Popadic kuchukua mikoba ya Hemed Suleiman ‘Morocco’ ambaye ana
majukumu ya kitaifa ya maandalizi ya timu ya Tanzania chini ya miaka 17, ‘Serengeti
Boys’.
Popadic
mwenye rekodi kubwa nchini alipokuwa akiwanoa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara (TPL), Simba SC ameungana na miamba ya soka katikati ya nchi
Singida United, kwa ajili ya kuongeza nguvu hususani kwa kipindi hiki cha
kuelekea Sportpesa Cup, ASFC na Ligi Kuu.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, anasema wanaimani na
makocha hao kuja kuleta mafanikio ndani ya kikosi hicho.
“Popadic
atakuwa kocha mkuu wa timu akisaidiwa na Dusan ambaye pia ni raia wa Serbia, kwa
kipindi cha mechi zaidi ya 10 Singida United imekuwa na matokeo yasiyoridhisha.
“Hivyo
wamiliki wa timu hiyo wameamua kuwapa kazi Waserbia hao ili kurejesha makali ya
kikosi hiki kilichofika fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) msimu uliopita,”
anasema.
Sanga
anasema; “Makocha walikuwepo na kikosi tayari wameshapewa taaarifa na
kukabidhiwa majukumu mengine ndani ya Singida United.”
No comments:
Post a Comment