Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi NMB, Manfred Kayala, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati wa droo ya nne ya promosheni ya matumizi ya Kadi za NMB MasterCard na Masterpass, ijulikanayo kama NMB MastaBata. (Picha na Francis Dande).
NA MWANDISHI WETU
DROO
ya nne ya promosheni ya matumizi ya Kadi za NMB MasterCard na
Masterpass, ijulikanayo kama NMB MastaBata, imefanyika mwishoni mwa
wiki, ambako wateja 26 wametangazwa washindi wa zawadi ya pesa na simu
janja {smartphone}.
NMB MastaBata ni promosheni
iliyozinduliwa Desemba 12 mwaka jana, ikilenga kuchagiza matumizi ya
malipo kwa kadi za MasterCard na Masterpass, ambako zawadi zenye thamani
ya Sh. Mil. 100 zimetengwa, ikiwemo zawadi kuu ya safari ya Dubai
iliyolipiwa kila kitu kwa washindi watatu na wenza wao.
Droo
ya nne ilifanyika mwishoni wiki katika Tawi la NMB Mlimani City jijini
Dar es Salaam, ambako wateja 20 walijishindia pesa Sh. 100,000 kila
mmoja, huku wengine sita wakijinyakulia 'smartphone' aina ya Samsung
Galaxy S9+.
Akizungumza wakati wa droo hiyo,
iliyochezeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania {GBT}, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi NMB, Manfred
Kayala, alisema, mwitikio miongoni mwa wateja wa Benki hiyo ni mkubwa na
kwamba kwa droo hiyo, wametimiza wiki nne zilizozalisha washindi 80 wa
Sh. 100,000 kila mmoja.
Kayala aliwataka wateja
wa NMB kuendelea kufanya malipo kwa kutumia NMB MasterCard na NMB
Masterpass, ili waweze kushinda mkwanja katika mwezi wa mwisho wa NMB
MastaBata, itakayofikia ukomo Februari 14.
"Wito
wetu kwa wateja wote ni kuendelea kufanya malipo kwa MasterCard na
Masterpass, ili kujishindia fedha, simu na zawadi kuu ya kulipiwa
gharama za safari ya kutembelea Dubai kwa washindi watatu na wenza wao
watakaowachagua," alisema Kayala.
No comments:
Post a Comment