Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano
Kusiluka, akizungumza na Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe waliohudhuria
warsha ya mabadiliko katika Sekta ya ajira kwa manufaa ya Jamii Afrika
Mashariki (TESCEA) inayoendelea Morogoro.
Washiriki wa warsha ya TESCEA katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi.
Mwezeshaji wa warsha hiyo toka nchini Kenya Prof. Charles Kingsburry akifafanua kuhusu mradi huo kwa Waandishi wa Habari
Na Mwandishi Wetu
Chuo Kikuu Mzumbe kupitia
mradi wake mpya wa ‘TESCEA’ kimeendesha warsha ya kuwajengea uwezo wahadhiri katika mbinu
bora za ufundishaji zinazosaidia wanafunzi kuweza kujiajirika pindi wanapohitimu masomo yao ya elimu ya juu.
Akizungumza katika uzinduzi wa warsha
hiyo inayoendelea katika hoteli ya
Morogoro, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lughano Kusiluka amesema Chuo Kikuu Mzumbe ni mahiri katika kufundisha
masomo ya biashara na menejimenti na sasa kinakwenda hatua ya mbele zaidi
kwakuwaandaa wahitimu wa ndani na hata nchi nyingine kutengeneza ajira kabla ya kuhitimu masomo yao.
Prof.Kusiluka ameeleza kuwa kumekuwa
na malalamiko mengi kutoka kwa waajiri dhidi ya wahitimu
wa vyuo vikuu nchini na kuonekana kutokuwa na
ujuzi wa kutosha na umahiri
katika fani walizosomea pindi wanapotaka kuajiriwa. Hivyo, Chuo Kikuu
Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo vikuu viwili kutoka Uganda (Uganda Martys na
Gulu), pamoja na asasi
za AFELT, LIWA, ASHOKA kutoka Kenya na
INASP kutoka Uingereza, wameanza kwa
kuwajengea wahadhiri ili kubadili mbinu
za ufundishaji zitakazowawezesha wahitimu kuwa na maarifa, ubunifu na ujuzi
zaidi kutambua na kutumia fursa
zilizopo ili kutengeneza ajira au kuajiriwa.
Kwa upande wake mwezeshaji wa warsha wa asasi ya umoja wa
Vyuo vikuu vinavyofundisha mbinu zinazohitajika katika kuboresha ufundishaji Afrika
Mashariki (AFELT) na Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Daystar cha Kenya Prof. Charles Kingsburry, amesema ni muhimu sasa kubadili mfumo wa
ufundishaji unaowafanya wahitimu kujua vitu kulingana na elimu wanayofundishwa
darasani pekee na kwa kutegemea mitandao ya intaneti na badala yake mbinu mpya
za ufundishaji ziwajenge katika ubunifu
,maarifa,mbinu na stadi halisia zitakazowawezesha kujiajiri wao na kuweza
kuajiri watu wengine. Hii ina lengo si tu la kuwafanya wahitimu kujua vitu tofauti
bali kuwajenga kuwa watu tofauti wanaoleta mabadiliko chanya kwa jamii nzima na
kujinufaisha wao na jamii zinawazunguka kupitia
elimu waliyopata.
Naye mwezeshaji mwingine toka Asasi ya AFELT na mhadhiri wa
Chuo Kikuu, Afrika Nazarene cha nchini Kenya Dkt. Kendi Muchungi amesema wahitimu
wa Vyuo Vikuu vyote vya Afrika Mashariki hawatofautiani na wamekuwa wakikosa uwezo
wa kujiajiri na kuajiriwa na hivyo
kushindwa kuisaidia jamii katika suala
la ajira kupitia elimu waliyopata, badala yake wamekuwa wakitegemea kuajiriwa. Hivyo ni imani yake kuwa mpango huo utaleta
mabadiliko kwa wahadhiri wa vyuo vikuu
katika ufundishaji na kunufaisha jamii
nzima ya Afrika Mashariki kupitia wasomi wachache.
Wakati huo huo mratibu wa Mradi wa ‘TESCEA’ kutoka Chuo Kikuu Mzumbe,Dkt.Albogast Musabila
amesema pamoja na lengo kuu la
mpango wa mradi huo la kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri na
kuajiri,Chuo Kikuu Mzumbe kwa
ushirikiano na wadau wa Sekta ya ajira, wahadhiri na wanafunzi kimeanza mchakato
wa kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya
kuandaa mapendekezo yatakayozingatiwa wakati wa kuboresha mitaala
na kuanzisha mitaala mipya.
No comments:
Post a Comment