HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 22, 2019

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA LEO IMEWASILISHA TAARIFA YAKE YA UTEKELEZAJI KWENYE KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo imewasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa bajeti kwa nusu mwaka ( Julai- Desemba, 2018) kwenye kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Mendeleo ya Jamii.

Taarifa hiyo ya Wizara imewasilishwa na Kaimu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe na imeainisha kazi zilizotekelezwa na Wizara ikiwa ni pamoja na kusajili jumla ya shule 163 kati ya 175 zilizoomba, Wizara imekagua jumla ya Asasi 11,327 zikiwemo shule za Msingi 8,785, Sekondari 2,480 na vyuo vya Ualimu 62.

Wizara pia imeandaa mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2018-  2021, kudahili sana huo 5842 waliojiunga na mafunzo ya Elimu ya Ualimu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kati ya 8,152 waliotarajiwa kujiunga na vyuo vya ualimu.

Prof. Mdoe pia ameieleza Kamati hiyo ya Bunge kuwa Wizara imeratibu skolashipu za wanafunzi wa vyuo Vikuu zinatolewa na nchi rafiki za Jumuiya ya Madola pamoja na nchi nyingine, kufuatilia Maendeleo ya udahili na uandikishaji wa wnafunzi katika Taasisi za Elimu ya Juu, kufuatilia utendaji wa vituo umahiri vya Afrika katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini.

Wizara pia imewezesha vyuo 20 vya Maendeelo ya Wananchi Kutoa Mafunzo ya Ufundi, kuzijengea uwezo taasisi za VETA, NACTE, na TCU ili kusimamia ubora wa Elimu ya Ufundi na stadi za Kazi.
 Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakiongozwa na Waziri Joyce Ndalichako wakimsikiliza mwenyekiti wa kamati. 
 Baadhi ya maofisa kutoka katika taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Elimu wakiwa katika kikao cha kamati.
 Wabunge wakiwa katika kikao hicho cha Kamati ya Bunge ya Huduma na Mendeleo ya Jamii.
 Baadhi ya maofisa kutoka katika taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Elimu wakiwa katika kikao cha kamati. 
wabunge wakifatilia mijadala.

No comments:

Post a Comment

Pages