HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 21, 2019

MAKINDA AWATAKA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA AFYA`

 Spika Mstaafu Anne Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Soko la Mchikichini Karume Ilala Dar es Salaam jana. Maadhimisho  hayo ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
 Spika Mstaafu Anne Makinda, akisalimiana na wakina mama baada ya kuwasili kwenye maadhimisho hayo.
 Spika Mstaafu Anne Makinda, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita.
 Wanawake na mabango yao katika hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Soko la Mchikichini-Ilala Jumanne Kongogo akizungumza kwenye maadhimisho hayo
 Mfanyabiashara na Mwezeshaji wa kisheria Jeonitha Katunzi akitoa ushuhuda jinsi walivyofaniwa kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Soko la Temeke Sterio baada ya kupatiwa mafunzo na EfG.
 Wasanii wakiigiza igizo la kupinga ukatili wa kijinsia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akihutubia.
 Wadau mbalimbali wakiwa meza kuu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), akimkabidhi machapisho mbalimbali, Spika Mstaafu Anne Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Soko la Mchikichini Karume Ilala Dar es Salaam jana. Maadhimisho hayo ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka yaliandaliwa na shirika hilo.
 Hapa ni furaha tupu katika maadhimisho hayo.
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Jinsia (UN-WOMEN), Lucy Tesha akitoa hutuba katika maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti wa muda wa Taifa wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara katika Masoko, Betty Mtewele , akimkabidhi Spika Mstaafu Anne Makinda zawadi ya batiki.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EfG, Penina Leveta akizungumza.
 Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa EfG.
Mgeni rasmi, Spika Mstaafu Anne Makinda, akiwaaga wanawake hao baada ya kumalizika kwa sherehe za maadhimisho hayo.

Na Dotto Mwaibale

SPIKA Mstaafu Anne Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) amewataka wanawake wajasiriamali nchini kujiunga na mfuko huo ili uweze kuwasaidia kupata matibabu pale wanakapokuwa wanaumwa.

Makinda ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo jana wakati akitoa hutuba kwenye Maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani yaliofanyika viwanja vya Soko la Mchikichini Karume Ilala jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)

"Wakina mama wajasiriamali changamkieni fursa ya kujiunga na NHIF utawasaidia kupata matibabu kwa bei nafuu pale mtakapo kuwa mnaumwa magonjwa mbalimbali" alisema Makinda.

Alisema hivi sasa gharama za matibabu katika hospitali mbalimbali ni za juu hivyo suluhisho pekee la kumudu gharama hizo ni kujiunga na mfuko huo ambao ni mkubwa hapa nchini.

Katika hatua nyingine Makinda amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuanzisha mpango wa vitambulisho kwa wajasiriamali kote nchini  kuwa vinawafanya wathaminiwe na kutambulika.

Alisema kupitia vitambulisho hivyo wajasiriamali wataweza kupata hata mikopo kupitia katika Halmashauri zao za wilaya walipo jambo ambalo ni zuri.

Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita akizungumzia mafanikio ya shirika hilo alisema mpaka sasa limeendesha program katika wilaya za Lushoto, Bumbuli, Ilala, Temeke, Ilemela, Nyamagana, Shinyanga Mjini, Shinyanga Vijijini, Jiji la Mbeya na 
mikoa mingine zaidi ya minne ambapo walitoa uhamasishaji wa program hiyo.

Alisema mafanikio waliyopata ni kuanzisha vikundi zaidi ya 30 vya Umoja wa wanawake katika masoko zaidi ya 35 nchini, kuwesha kuundwa kwa vikundi 58 vya kuweka na kukopa (VICOBA), wanawake zaidi ya 70 wameshika nafasi mbalimbali za 
uongozi sokoni.


No comments:

Post a Comment

Pages