Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi wakati wa ziara katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, jijini Dar es Salaam ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli
kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo
hicho. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Askari
Polisi ambao ni wanafunzi katika Chuo cha Taaluma ya Jeshi la Polisi, wakati alipotembelea chuoni hapo kufuatilia maandalizi ya awali baada ya jeshi hilo kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba
kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.Ziara hiyo
imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi
Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa
majengo ya chuo hicho, kulia ni Mkuu wa Chuo, Naibu Kamishna, Anthony Rutashuburugukwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi
Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho,Wengine ni viongozi wa chuo.
Na
Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi nchini limeelekezwa
kutumia wafungwa ili kuweza kuokoa kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili kati ya Milioni Mia Saba zilizotolewa na Rais
Dk. John Magufuli katika Mradi wa Ujenzi wa Mabweni na Madarasa
ya Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Maelekezo hayo
yametolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
alipotembelea majengo chakavu ya chuo hicho baada ya kupokea kiasi cha Shilingi
Milioni Mia Saba alizoahidi Rais Dkt. John Magufuli akihutubia katika mahafali
ya kuhitimisha Mafunzo ya Kozi za Uofisa na Ukaguzi Msaidizi chuoni hapo mwishoni mwa mwaka jana
“Wizara ina taasisi ya
magereza ambayo ina nguvu kazi ya kutosha, na Rais alishaagiza wafungwa
watumike katika shughuli za uzalishaji, sioni sababu ya kutumia kiasi hicho cha
pesa kuwalipa vibarua wa nje, naagiza muwasiliane na Jeshi la Magereza pamoja
na kikosi cha ufundi kilichopo ndani ya Jeshi la Polisi ili muweze kuona ni
vipi mnaokoa kiasi hicho”alisema Masauni
Akitoa taarifa ya awali
ya ujenzi huo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi, Naibu Kamishna Anthony Rutashuburugukwa
alitaja majengo yatakayojengwa kuwa ni
ghala la chuo, madarasa matatu,bweni moja la askari wa kiume na bweni lingine la
askari wa kike.
Wakizungumza kwa
masharti ya kutotajwa majina wanafunzi wa chuo hicho walimshukuru Rais Dkt.
Johh Magufuli kwa kiasi cha fedha
alichotoa ili kuweza kujenga sehemu mbalimbali za chuo hicho ikiwemo mabweni
ambayo wamekiri ni chakavu na si rafiki kwa matumizi ya binadamu.
No comments:
Post a Comment